◾️قال ابن القيم رحمه الله:
Amesema ibn l-Qayyim – Allah amrahamu – :
- سمعت شيخ الإسلام ابن تيمية يقول : إذا لم تجد للعمل حلاوة في قلبك وانشراحًا فاتهمه،
Nimemsikia sheikh l-islam ibn Taimiyyah akisema : kama haujakuta raha katika moyo, na ukunjufu wa kifua kwa ibada (uliyoitenda) basi utuhumu huo (moyo),
فإنّ الرب تعالى شكور،
Kwa sababu Mola mlezi ni mwingi wa shukurani,
يعني أنه لا بد أن يثيب العامل على عمله في الدنيا من حلاوة يجدها في قلبه، وقوة انشراح، lوقرة عين، فحيث لم يجد ذلك فعمله مدخول.
Maana yake kwamba yeye (Allah) ni lazima amlipe mtendaji (ibada) juu ya ibada yake katika (hii) dunia, (kwa kumpa) ladha atakayoipata moyoni mwake, na nguvu ya ukunjufu wa kifua, na kiburudisho cha macho, na pale (ambapo) hakuyapata (haya) basi ibada zake (anazozifanya) zimeingiliwa.
📚 [مدارج السالكين (٥١/٢)
Maelezo ya mfasiri :
Miongoni mwa majina ya Allah ni الشَّكُوْرُ ambalo tafsiri yake kwa Kiswahili ni mwingi wa shukurani, na maana na makusudio yake kama alivyosema ibn Kathir Asshafiy – Allah amrahamu – pindi alipokuwa anatafsiri aya ya 17 katika suratu-Ttaghabun :
( وَاللّٰهُ شَكُوْرٌ )
{Na Allah ni mwingi wa shukurani…}
أي : يجزي على القليل بالكثير
Maana yake : Hulipa juu ya kichache (kilichotendwa) kwa (kutoa thawabu) nyingi.
Kwa hiyo shukurani ya Allah ni kule kuridhia kwake twaa (ibada) chache kutoka kwa mja na kuzikubali.
Ikiwa ni hivyo basi ndiyo maana hapa sheikh – Allah amrahamu -akasema kuwa ikiwa muislamu hahisi raha katika ibada anazozifanya basi aikague nafsi yake na aituhumu, na ajue kuwa ibada zake zimeingiliwa na yale yenye kuzichafua hizi ibada kama vile : Kujionesha, kutafuta sifa, n.k.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 7, 1445H ≈ Nov 21, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•