KAMA UPO HIVI BASI JIREKEBISHE!

▪️ الفارغُ القلب من الله والدار الآخرة، المُبتلى بمحبة الدنيا ،

(Yule ambaye) moyo wake umeepukana na Allah, na nyumba ya akhera, aliyepewa mtihani wa kuipenda dunia,

أشقّ ما عليه الصلاة، وأكرهُ ما إليه طُولها.

(Kitu) kizito zaidi kwake ni swala, na kinachochukiza zaidi kwake ni (ule) urefu wake hiyo (swala)

📚 رسالة ابن القيم إلى أحد إخوانه صـ ٣٩

Maelezo ya mfasiri :

Ukiiona nafsi yako ni nzito katika swala, na unachukia kuswali swala ndefu basi hiyo ni ishara ya kuwa umemtoa Allah katika moyo wako na umefitinika na kuipenda dunia, na tiba yake ni kukithirisha kumtaja Allah na kumkumbuka, na pia kukithirisha kumkumbuka kifo kwa ajili ya kujiandaa na hicho kifo kwa kufanya matendo mema, pia itambulike kuwa kuwa mvivu katika swala ni katika sifa za wanafiki, kama alivyosema Allah _aliyetukuka – :

إِنَّ ٱلْمُنَٰفِقِينَ يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَهُوَ خَٰدِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوٓاْ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ قَامُواْ كُسَالَىٰ يُرَآءُونَ ٱلنَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ ٱللَّهَ إِلَّا قَلِيلًا

Hakika wanafiki wanamkhadaa Allah ,na hali yeye (Allah) ni mwenye kuwakhadaa wao.Na wanaposimama kuswali husimama kwa uvivu ,wanawaonesha watu (kuwa wanaswali) wala hawamtaji Allah ila kidogo .

النساء : ١٤٢

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane  13, 1445H ≈ Nov 27, 2023M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *