كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .
Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :
العقل وعاءٌ، واللِّسان آلةٌ تؤدِّي عنه،
Akili ni chombo, na ulimi ni kifaa kinachofanya kazi kwa niaba ya hiyo (akili),
فإذا أردتَ أن تعرف قدر عقلٍ أحدٍ؛ فانظر إلى ما يتكلَّم به،
na ukitaka kujua kiwango cha akili ya yeyote , basi angalia kile anachokizungumza,
وصفة كلامه، وزمانه، ومكانه،
na sifa ya maneno yake,na wakati wake,na sehemu yake,
فما خفي من العقل؛ يفصح عنه اللِّسان، ويدلُّ عليه.
basi kile kilichojificha katika akili huwekwa wazi na ulimi na (ulimi) huijulisha hiyo (akili).
الخميس 9 جمادى الأولى ١٤٤٥
Maelezo ya mfasiri:
Akili ya mtu hudhihiri katika ulimi wake kwa sababu ulimi hutamka kile kinachotoka akilini mwa mtu ,na mwenye akili hazungumzi ovyo ila kabla ya kuzungumza huchunguza na kufikiria faida na hasara ya hayo maneno, kwa ajili hii sifa ya maneno yake huwa ni nzuri, na maneno yake huendana na muda na wakati aliopo kwa sababu maneno huwenda yakawa mazuri lakini yanapozungumzwa wakati usiostahiki hayawi mazuri pengine huwenda yakaleta madhara , na pia eneo la mazungumzo huwenda maneno ni mazuri lakini yakawa ni mabaya katika baadhi ya maeneo kwa maana hayastahiki kuzungumzwa maeneo hayo pamoja na uzuri wake.
Ufupi wa ujumbe wa sheikh ni huu :
Ikiwa hatujui akili ya mtu basi tuangalie maneno yake kwa sababu maneno hufichua akili ya mtu na kuibainisha .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 6, 1445H ≈ Dec /19, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•