قول الحافظ ابن كثير – رحمه الله – في “تفسيره” عن نبي الله عيسى بن مريم – عليه السلام -:
Ni kauli ya Al-hafidh ibn Kathir -Allah amrahamu-katika tafsiri yake kuhusu nabii Isa bin Mariam -amani iwe juu yake-:
«وكان أول كلمة نطق بها وهو صغير في المَهد أنْ قال:
Na yalikuwa maneno ya mwanzo aliyoyatamka na hali yeye ni mtoto (mchanga) kitandani alisema (hivi):
{ إِنِّي عَبْدُ اللَّهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا}
“Hakika mimi ni mja wa Allah,Amenipa kitabu na Amenifanya Nabii”
ولم يقل:
Na hakusema :
أنا الله، ولا ابن الله.
Mimi ni Mwenyezi Mungu wala mimi ni mtoto wa Mwenyezi Mungu .
إلى أنْ قال:
mpaka aliposema:
{ وَإِنَّ ٱللَّهَ رَبِّى وَرَبُّكُمْ فَٱعْبُدُوهُ ۚ هَٰذَا صِرَٰطٌ مُّسْتَقِيمٌ }
Na hakika Allah ni Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi .Basi muabuduni.Hii ni njia iliyonyooka.
مريم 36
Maelezo ya mfasiri:
Huu ni ushahidi wa wazi juu ya upotevu wa dini ya kinaswara ambayo miongoni mwa itikadi zake ni kuamini kuwa Isa bin Mariam -amani iwe juu yake-ni mtoto wa Mwenyezi Mungu au yeye mwenyewe ndiye Mungu ,au ni mmoja katika miungu mitatu wanayoiamini hao Manaswara ,na Mwenyezi Mungu ametakasika na yote hayo wanayoyazungumza makafiri .
Isa bin Marym -amani iwe juu yake- yeye ni mja wa Allah na hilo ni neno lake la mwanzo kutamka baada ya kuzaliwa tu , neno ambalo linabatilisha itikadi ya Manaswara ya kuamini kuwa yeye ndiye Mungu au mtoto wa Mungu au ni mmoja katika Miungu mitatu wanayoiamini Manaswara na yote haya ni upotevu na ukafiri, na itikadi sahihi kwa Isa bin Marym ni kuamini kuwa yeye ni mja wa Allah na ni mtume katika mitume yake .
Tanbih:
Maneno haya yameandikwa na sheikh Abdul-Qadir Al-junaid-Allah amuhifadhi- , ila mimi nimeyaingiza katika lugha ya kiswahili na kuweka maelezo .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 12, 1445H ≈ Oct 25, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•