DARAJA ZA KISIMAMO CHA KUUTAFUTA USIKU WA CHEO

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: http://www.fawaidusalafiya.net

DARAJA ZA KISIMAMO CHA KUITAFUTA LAILATUL- QADIR (USIKU WA CHEO)

مراتب قيام ليلة القدر المستحبة أربعة:

Daraja za kusimama usiku wa cheo zilizosuniwa ni nne:

١- المرتبة الأولى : أن يقوم الليل كله.

٢- المرتبة الثانية: أن يقوم أول الليل وآخره.

٣- المرتبة الثالثة: أن يقوم آخر الليل فقط.

٤-المرتبة الرابعة: أن يقوم أول الليل فقط.

1 – Daraja la kwanza: Ni kusimama usiku wote.

2 – Daraja la pili: Ni kusimama mwanzoni mwa usiku na mwishoni mwake.

3 – Daraja la tatu: Ni kusimama mwishoni mwa usiku pekee.

4 – Daraja la nne: Ni kusimama mwanzoni mwa usiku pekee.

Ufafanuzi:

Hizi ni daraja nne za kusimama katika siku hizi za kuutafuta usiku wa cheo, nazo ni nne:

1 – mtu akasimama usiku wote kwa kuswali au kusoma quran, kuomba dua, kumtaja Allah.

2 – Mtu akasimama mwanzoni mwa usiku kadri ya uwezo wake, kisha akasimama tena mwishoni mwa usiku (kabla ya al-fajir) kadri ya uwezo wake.

3 – Mtu akasimama mwishoni mwa usiku pekee (akalala kisha akaamka).

4 – Mtu akasimama mwanzoni mwa usiku pekee yaani baada ya swala ya ishaa,

Na daraja kubwa zaidi katika hizi ni: Daraja la kwanza kisha la pili, kisha la tatu kisha la nne.

Ukamilifu zaidi kwa mja ni kuziimarisha hizi siku kumi ambazo zinatarajiwa ndani yake usiku wa cheo, aziimarishe kwa swala, kwa kusoma qurani, kwa kuomba dua na kukaa itikafu msikitini.

Kama halikumwezekania hilo inapendeza asimame mwanzoni mwa usiku na mwishoni mwake, aswali kadri anavyoweza, asome (qurani) aombe dua, kadri ya uwezo wake kisha afanye hivyo mwisho wa usiku (kabla ya al-fajiri).

Na kama hakuliweza hili na akaweza moja ya ncha mbili za usiku basi bila shaka (kusimama) kwake mwishoni mwa usiku ni ukamilifu zaidi kuliko mwanzoni mwa usiku, basi (yaani) aicheleweshe swala yake mpaka mwishoni mwa usiku basi huu ni ukamilifu zaidi kuliko yule anayetosheka na (ibada) mwanzoni mwa usiku.

Faida:

Maana ya kauli ya Allah -aliyetukuka-:

{ لَيْلَةُ ٱلْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍۢ }

{Usiku wa cheo ni bora kuliko miezi elfu } .

ufafanuzi:

Maana ya aya hii kuwa matendo yanayofanywa katika usiku huo yakikubaliwa na Allah yanalingana na matendo ya miezi elfu moja ambayo ni sawa na miaka 83 na miezi 4 ,ambayo haina usiku wa cheo .

Na Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- amefafanua matendo yanayofanywa usiku huo akasema :

“مَنْ قَامَ لَيْلَةَ الْقَدْرِ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ”

” Mwenye kusimama usiku wa cheo hali ya kumuamini Allah na hali ya kutaraji malipo kutoka kwa Allah atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake “

رواه البخاري ومسلم .

Uchanganuzi :

Hadithi imeeleza matendo yanayofanywa usiku huo nayo ni : Kuswali ,na kunaingia ndani yake kusoma qurani ,nyiradi mbalimbali ,kuomba dua ,kukaa itikafu ,haya ndiyo matendo yanayofanywa usiku huo, na ujira wake ni kusamehewa madhambi yake yaliyopita .

Chimbuko:

Hii ni sehemu katika muhadhara alio utoa Sheikh Swaleh Al-Uswaimiy – Allah amuhifadhi – muhadhara wenye faida nyingi kuhusu hili kumi la mwisho, na hayo maelezo pia yanatokana na maneno ya Sheikh, kwa maana mimi nimetafsiri tu na kuyaweka katika mfumo huu ili manufaa yaenee kwa ndugu zangu waislamu.

Muandaaji: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshaafi’iy

Tembelea website yetu: ☟
http://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Ramadhani 22, 1442H ≈ May 4, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *