قال الفضيل بن عياض-رحمه الله – :
Amesema Al-fudhail bin ‘Iyadh -Allah amrahamu-:
إذا ظهرت الغيبة ارتفعت الأخوة في الله.
Kutakapodhihiri usengenyi, huondoka undugu kwa ajili ya Allah
إنما مثلكم في ذلك الزمان .
Hakika si vingine mfano wenu wakati huo .
مثل شيء مطلي بالذهب والفضة داخله خشب وخارجه حسن.
Ni mfano wa kitu kilichopakwa (rangi) ya dhahabu na fedha (lakini) ndani yake ni mbao, na nje yake ni (kitu) kizuri .
📚 حلية الأولياء 8-96
Maelezo ya mfasiri:
Amesema kweli Fudhail-Allah amrahamu- hili limesadikishwa na matukio, kana kwamba huo wakati anaouzungumzia ni huu , ni wangapi katika waislamu waliopendana kwa ajili ya Allah na wakatengana kwa sababu ya usengenyi ?!, na hivi hivi ndivyo walivyo baadhi ya waislamu wa zama hizi wapo kama mbao zilizopakwa rangi ya dhahabu na fedha kwa nje zinang’aa na kuvutia Kama dhahabu na fedha lakini si dhahabu wala fedha bali ni mbao tupu!, huu ni mfano wa jamii ambayo usengenyi umekithiri ndani yake .
Na bila shaka usengenyi ni dudu baya ambalo likiingia katika jamii fulani hutafuna tafuna kila kitu, kwa sababu kawaida mtu anapojua kuwa fulani ananisengenya basi hujenga chuki moyoni mwake na matokeo yake ni kuenea chuki baina yao , na ukitaka kujua ubaya wa usengenyi tosheka tu na maneno yake Allah pale alipoifananisha na dhambi hii na mtu kula nyama ya ndugu yake aliyefariki :
وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ
Wala baadhi yenu wasiwasengenye wengine.Je !Mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa ? La, Hampendi ; (Basi haya msiyapende). Na mcheni Allah .Bila shaka Allah ni Mwingi wa kupokea toba (na) Mwingi wa kurehemu .
سورة الحجرات 12.
Tafsir ya sheikh Al-farsy -Allah amrahamu- .
Na usengenyi maana yake ni kama alivyoeleza Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- :
”ذِكْرُك أخاك بما يَكْرَهُ “
“ Kumtaja kwako ndugu yako kwa yale anayoyachukia ”.
أبو داود (4874).
Na wema waliopita walikuwa wanajiepusha mno na tabia hii ya usengenyi ,basi sisi tunaojinasibisha nao tunatakiwa tuwe mstari wa mbele katika kujiepusha na tabia hii chafu , lakini kwa masikitiko wapo watu tena muonekano wao ni wa dini lakini wanasifika na tabia hii chafu .
قال ابن الجوزي- رحمه الله- واصفًا شيخه عبدالوهاب الأنماطي:
Amesema ibn Al-jauziy- Allah amrahamu- akimsifu sheikh wake Abdul-Wahhab An-Matwiy -:
“كان على قانون السلف لم يُسمع في مجلسه غيبة…”؛
“ (Huyu sheikh) alikuwa (anafuata) kanuni za wema waliopita, hakujasikika katika vikao vyake usengenyi ..”
(صيد الخواطر: ص: 173).
Tunamuomba Allah atuepushe na tabia hii chafu na atupambe na tabia njema .
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 7 , 1445H =Apr 16, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•