MALIPO KWA WENYE KUYADHIHAKI MANENO YA MTUME- SWALA NA SALAMU ZA ALLAH ZIMFIKIE-

قال ابن القيم رحمه الله:

Amesema ibn l-Qayyim-Allah amrahamu-:

وقال أحمد بن مروان المالكي في كتاب «المجالسة» له:

Amesema Ahmad bin Mar-wan Al-malikiy katika kitabu chake “Al-mujaalasah” :

حدثنا زكريا بن عبدالرحمن البصري،قال :

Ametusimulia Zakaria bin Abdul-Rahman Al-basry amesema :

سمعت أحمد بن شعيب يقول:

Nimemsikia Ahmad bin Shu’ab akisema:

كنا عند بعض المُحدّثين بالبصرة فحدّثنا بحديث النبي ﷺ:

Tulikuwa kwa baadhi ya wanavyuoni wa hadithi (katika mji wa) Basrah basi akatusimulia hadithi ya Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-:

«إن الملائكة لتضع أجنحتها لطالب العلم … »،

“Hakika Malaika huweka mbawa zao kwa mwenye kutafuta elimu…”

وفي المجلس معنا رجل من المعتزلة، فجعل يستهزئ بالحديث،

Na katika (hiki) kikao kulikuwa na mtu (mmoja) katika (pote) la Mu’utazilah, basi akaanza kuidhihaki hadithi,

فقال: والله لأطرقنّ غدا نعلي بمسامير، فأطأُ بها أجنحة الملائكة! ففعل،

na akasema (hivi): Namuapia Allah, kesho nitagongea misumari viatu vyangu ili nizikanyage mbawa za Malaika ,na (kweli) akafanya hivyo,

ومشى في النعلين؛ فجفّت رجلاه جميعا، ووقعت في رجليه الآكلة.

na akatembelea viatu vyake hivyo ,basi miguu yake yote miwili ikakauka, na (pia hiyo) miguu yake ikapatwa na maradhi ya kutafunika .

وقال الطبراني: سمعتُ أبا يحيى زكريا بن يحيى الساجي قال:

Na amesema Attwabaraniy :

Nilimsikia Abuu Yahya Zakariyyah bin Yahya Assajiy alisema :

كنا نمشي في بعض أزقة البصرة إلى باب بعض المُحدّثين، فأسرعنا المشي،

Tulikuwa tukitembea katika baadhi ya vinjia vidogodogo vya Basrah tukielekea katika mlango wa baadhi ya wanavyuoni wa hadithi,

وكان معنا رجل ماجن متّهم في دينه، فقال:

na tulikuwa pamoja na mtu mmoja mjinga mwenye kutuhumiwa katika dini yake ,basi (yule mtu) akasema:

ارفعوا أرجلكم عن أجنحة الملائكة لا تكسروها! كالمُستهزئ،

Nyanyueni miguu yenu (muiepushe na) mbawa za Malaika musizivunje ! (alizungumza hivyo) kwa kufanya dhihaki

فما زال في موضعه حتى جفّت رجلاه وسقط.

basi aliendelea kubakia sehemu yake (ileile aliyokanyaga) mpaka miguu yake ikakauka na akadondoka .

📚 مفتاح دار السعادة (٢٥٦/١ – ٢٥٧)

Maelezo ya mfasiri:

Yapo matukio mengi yaliyotokea kwa wale waliozidhihaki suna za Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- na watu hawa wapo mpaka leo hii ambao wao huzidharau na kuzidhihaki suna za Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- mfano kuna wale wanaozidhihaki ndevu kwa kusema kuwa ni uchafu ! , au mavazi yasiyofunika kongo mbili na kuyaita ni vipedo! , watu hawa wanatakiwa wawe na tahadhari wasije wakaingia katika ukafiri au kuanza kuadhibiwa hapa hapa dunia kabla ya akhera, kama walivyoadhibiwa hao waliotajwa hapa kwa sababu ya kuyadhihaki kwao maneno ya Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- maneno ambayo yamethibiti katika hadithi ndefu ambayo ndani yake kuna maneno haya :

وإنَّ الملائكةَ لتضعُ أجنحتَها رضًا لطالبِ العِلمِ ،

Na hakika Malaika huweka mbawa zao (kwa mwenye kutafuta elimu) kwa kumridhia (huyo) mwanafunzi..

رواه أبو دود وغيره .

Kipande hiki cha hadithi kinaelezea ubora wa mwanafunzi wa elimu ya kisheria, mpaka Malaika humuwekea mbawa zao na yeye hutembea juu ya hizo mbawa, au maana yake hao Malaika huzizuia mbawa zao na kuteremka katika vikao vya elimu ili kusikiliza , hivi ndivyo walivyoeleza wanawavyuoni.
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 8 , 1445H =Apr 17, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *