◾️ قال شيخ الإسلام ابن تيمية رحمه الله:
Amesema sheikh l-islam ibn Taimiyyah- Allah amrahamu-:
” والذنوب تنقص الإيمان، فإذا تاب العبد أحبه الله، وقد ترتفع درجته بالتوبة؛ قال بعض السلف:
Na madhambi yanapunguza imani, na mja anapoleta toba Allah humpenda,na huwenda daraja lake likanyanyuka (zaidi) kwa sababu ya kuleta toba,wamesema baadhi ya (wema) waliopita:
(كان داود بعد التوبة خيرا منه قبل الخطيئة).
(Nabii) Daud baada ya kutubia akawa ni mbora zaidi kuliko (alivyokuwa) kabla ya kukosea.
- فمن قضي له بالتوبة كان كما قال سعيد بن جبير:
Basi yule aliyekadiriwa (aliyewepesishiwa) kutubia atakuwa kama alivyosema Said bin Jubair:
(إن العبد ليعمل الحسنة فيدخل بها النار وإن العبد ليعمل السيئة فيدخل بها الجنة؛ وذلك أنه يعمل الحسنة فتكون نصب عينه ويعجب بها، ويعمل السيئة فتكون نصب عينه فيستغفر الله ويتوب إليه منها)”.
Hakika mja hufanya jema na huingia motoni kwa sababu (jema) hilo, na hakika mja hufanya uovu na huingia peponi kwa sababu ya (uovu) huo, na hilo ni kwamba yeye hufanya jema na (hilo jema) huliona kuwa ndiyo kila kitu ,na hujiona (hujivuna) kwa hilo (jema alilolifanya), na (mwengine) hufanya uovu na hujiona kuwa amefanya kosa kubwa,basi humtaka msamaha Allah na huleta toba kutokana na kosa hilo .
📚 مجموع الفتاوى (١٠\٤٥).
Maelezo ya mfasiri:
Hiyo ndiyo maana ya maneno hayo ya kuwa mtu anaweza akafanya mema na ikawa ni sababu ya kuingia motoni kwa wema huo ni kwa sababu ya kule kujiona kwake na kujivuna kwa hayo mema anayofanya ! , na mwingine anaweza akafanya dhambi ikawa hiyo dhambi ni sababu ya kuingia peponi na huyu ni yule ambaye baada ya kujua kuwa amemkosea Allah akawa anajuta kwa kule kuifanya ile dhambi,na akarudi kwake na akaleta toba na kumuomba msamaha Allah,na mja anapomtaka msamaha Allah na kutubu kwake baada ya kufanya dhambi hali yake huwa ni bora zaidi ya vile alivyokuwa kabla ya kufanya dhambi, kama ilivyokuwa kwa nabii Daud -amani iwe juu yake- yeye baada ya kukosea na akamtaka msamaha Allah na kurudi kwake basi ubora wake ukaongezeka , amesema Allah aliyetukuka namna Daud- amani iwe juu yake- alivyomtaka msamaha Allah :
ۗ وَظَنَّ دَاوُودُ أَنَّمَا فَتَنَّاهُ فَاسْتَغْفَرَ رَبَّهُ وَخَرَّ رَاكِعًا وَأَنَابَ ۩
« Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani (ili azinduke). Basi akamuomba msamaha Mola wake,na akaanguka kusujudu na kutubia»
سورة ص 24
Faida :
Ama kuhusu dhambi gani aliyoifanya Daud-amani iwe juu yake- kuna maneno mengi yamezungumzwa katika hili, na mengine ni uwongo kabisa yanayopingana na nafasi yake ya utume na yafuatayo ni maneno ya mwanawachuoni mkubwa Abdul-Rahman bin Si’id -Allah amrahamu- katika hili:
“هذا الذنب الذي صدر من داود عليه السلام لم يذكره الله لعدم الحاجة إلى ذكره،
Hii dhambi ambayo iliyotoka kwa Daudi-amani iwe juu yake- Allah hakuitaja kwa sababu ya kutokuwa na haja ya kutajwa,
فالتعرُّض له من باب التكلُّف، وإنما الفائدة ما قصَّه الله علينا من لطفه به، وتوبته وإنابته،
Na kuikusudia (kuijua) ni katika mlango wa kujipa shida, na hakika si vingine faida (ipo) katika yale aliyotusimulia Allah katika upole wake kwa huyo (Daudi) na kutubia kwake na kurejea kwake kwa (Allah)
وأنه ارتفع محله، فكان بعد التوبة أحسن منه قبلها”؛
Na kwamba yeye (Daudi) amenyanyuka (kidaraja) na akawa baada ya kuleta toba, hali yake ikawa nzuri zaidi ya vile alivyokuwa kabla ya huko (kutubia) .
((تفسير السعدي)) (ص: 712).
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 14 , 1445H =Apr 23, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•