FAIDA YA KITABIBU KWA WENYE WATOTO WACHANGA.

قال ابن القيم رحمه الله تعالى:

Amesema ibn l-Qayyim-Allah aliyetukuka amrahamu-:

” وينبغي أن يُقْتَصر بهم على اللبن وحده إلى نبات أسنانهم ،

Inatakikana patoshekwe na (kuwapa) maziwa pekee mpaka (wakati) wa kuota meno yao ,

لضعف معدتهم وقوتهم الهاضمة عن الطعام،

kwa sababu ya udhaifu wa vifuko vyao vya chakula na (kutokuwa) na nguvu ya kumeg’enya chakula ,

فإذا نبتت أسنانه قويت معدته، وتغذى بالطعام،

Na yaotapo meno yake kifuko chake cha kuhifadhia chakula hupata nguvu ,na (muda huo sasa) hula chakula,

فإن الله سبحانه أخَّر إنباتها إلى وقت حاجته إلى الطعام لحكمته ولطفه،

basi bila shaka Allah-utakasifu ni wake- amechelewesha uotaji wa hayo (meno) mpaka afike wakati wa kuhitajia chakula kwa hekima zake na huruma zake

ورحمة منه بالأم، وحلمة ثديها فلا يعضه الولد بأسنانه.

na ni huruma itokayo kwake (Allah) kumhurumia mama, na chuchu ya matiti yake asije mtoto akaing’ata kwa meno yake.

وينبغي تدريجهم في الغذاء، فأول ما يطعمونهم: الغذاء الليِّن،
Na inatakikana kuwapa chakula hatua kwa hatua ,cha mwanzo wanachowalisha ni chakula laini,

فيطعمونهم الخبز المنقوع في الماء الحار، واللبن والحليب،

wawalishe (kama vile) mkate uliolowekwa katika maji ya moto ,na maziwa ya mama na maziwa fresh,

ثم بعد ذلك الطبيخ، والأمراق الخالية من اللحم،

kisha baada ya (vyakula) hivyo (wawape vyakula) vinavyopikwa na michuzi isiyokuwa na nyama ,

ثم بعد ذلك ما لطف جدا من اللحم بعد إحكام مضغه، أو رضه رضا ناعما “.

Kisha baada ya (vyakula) hivyo (wawape) zile zilizokuwa nyepesi katika nyama baada ya kuzitafuna vizuri au baada ya kuziponda upondaji wa (kuzifanya) kuwa nyororo

تحفة المودود بأحكام المولود” (ص 339).

Maelezo ya mfasiri:

Allah amrahamu ibn l-Qayyim kwa faida hii katika upande wa malezi ya watoto, Allah amrahamu mwanawachuoni huyu ambaye amefariki mwaka 751 baada ya hijra naye ni miongoni mwa wanawavyuoni ambao Allah amewaruzuku elimu ya tiba pia, kama walivyoruzukiwa elimu ya kisheria .

Hapa ameeleza ibn l-Qayyim -Allah amrahamu- kuwa mtoto asipewe chochote kabla ya kuota meno isipokuwa maziwa tu, na mimi nilimuuliza mmoja katika madaktari (Abuu Imraani) akaniambia kuwa : Maziwa ya mama yana protin nyingi ambayo humsaidia sana mtoto katika ukuaji kama vile kuimarisha ubongo wake kwa haraka, na kinga za mwili zinakuwa imara zaidi kwa hayo maziwa ya mama, na daktar mwingine Abuul-faruq yeye aliniingezea faida akaniambia kuwa maziwa ya mama yana kila kitu kinachohitajika kwa mtoto kwa ile miezi sita ya mwanzo ndiyo maana hata katika vituo vya kutolea huduma za afya hushauri watoto wanyonyeshwe maziwa ya mama pekee kwa miezi sita.Hili lina faida nyingi za kiafya kwa mama na mtoto. Ama baada ya kukuwa mtoto anakuwa ameimarika hata mfumo wake wa umeng’enyaji unakuwa unauwezo wa kumeng’enya hivyo vyakula, ndiyo maana anapofika umri wa kuota meno hupewa chakula na ibn l-Qayyim-Allah amrahamu- pia akaeleza hekima ya hilo la kutopewa chakula kabla ya kuota meno, kisha akaeleza kuwa mtoto anapofikia umri wa kuanza kula anatakiwa apewe vyakula kwa hatua na akavitaja kutokana na vyakula vilivyopo katika zama zake na vile anavyovijua yeye :

1-Apewe vyakula laini, akatoa mfano wa vyakula laini : Mkate uliolowekwa katika maji ya moto na maziwa pia aendelee kunyonya.

2-Kisha apewe vyakula vilivyopikwa, na wapewe pia michuzi mitupu bila ya nyama kwa maana achemshe nyama au samaki kisha ampe mchuzi wake .

3- Kisha apewe nyama laini baada ya kumtafunia au kuziponda vizuri na amesema hivyo kutokana na zama alizokuwa akiishi kipindi hicho mama alikuwa akimtafunia mwanawe chakula ili kumlainishia au kumpondea kwa zana zilizopo kipindi hicho ama katika zama tulizopo Allah -aliyetukuka- ameleta wepesi wa kuwepo brender kifaa ambacho kinawepesi wa kusaga chakula mpaka kikawa laini kabisa- sifa zote njema ni za Allah -.

•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 15 , 1444H =Apr 24, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *