➡️ Makala namba (26)
↩️ وهو الاستسلام لله بالتوحيد.
🌱Na huo (Uislamu): Ni kujisalimisha kwa Allah kwa kumpwekesha.
↩️والانقياد له بالطاعة
↩️ والبَرَاءَةُ مِنَ الشِّركِ وَأَهْلِهِ).،
🌱na kumfuata kwa kunyenyekea kwa kutii .
🌱na kujitenga mbali na ushirikina na watu wake.
✍️Sherhe inayotokana na wanawachuoni mbalimbali:
ೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐ ೄ
shekh-Allah amrahamu- aliposema:
“Uislamu ni kujisalimisha kwa Allah kwa kumpwekesha “.
Maana yake ni Kumuabudu Allah pekee, na mwenye kumuabudu Allah pekee bila ya kumshirikisha na choche basi huyo amejisalimisha kwake.
Kwa hiyo uislamu ni mtu kuusalimisha uso wake na makusudio yake na niya yake kwa Allah aliyetukuka amesema Allah aliyetukuka:
{وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَٱتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَٰهِيمَ حَنِيفًا ۗ }
“ Na nani aliye mbora zaidi kwa dini kuliko yule ambaye ameuelekeza uso wake kwa Allah, naye ni mwema, na anafuata mila ya Ibrahim (kuwa muislam kweli kweli).
Annisa 125
Tukiyazingatia maneno ya sheikh hapa tutafahamu kuwa mtu hawi muislam mpaka kukusanyike kwake mambo yafuatayo :
1️⃣ Kujisalimisha kwa Allah kwa kumuabudia yeye pekee bila ya kumshirikisha na chochote.
2️⃣ Kumnyenyekea Allah kwa kumtii.
3️⃣ Kujitenga na yale yanayoenda kinyume na kumpwekesha Allah na kumtii nayo ni ushirikina.
4️⃣ Kujitenga mbali na washirikina.
Mtu ambaye kumethibiti kwake mambo haya manne basi huyo ni muislam ama yule ambaye imepungua kwake moja katika sifa hizi basi mtu huyo si muislamu.
Tanbih:
Makusudio ya kujitenga mbali na ushirikina na watu wake (washirikina) hapa ni kuuchukia ushirikina na washirikina, na asili ya kuchukia ni ipo moyoni na yanayofuata baada ya kuwachukia ni :
1-Kuwafanyia uadui hao washirikina
2- Kuwakufurisha wale waliokufurishwa na Allah na Mtume wake-swala na salamu za Allah zimfikie- .
3- Kupigana nao au kupambana nao pindi kutakapo thibiti jihad ya kisheria .
Ama watu wa kawaida ambao hawajishughulishi na elimu wao wanawajibika kuuchukia ushirikina na washirikina ama hayo matawi yake tuliyoyataja hapo juu yatawajibika kwa muislamu baada ya kuyafahamu .
Kwa hiyo ifahamike kuwa kuuchukia ushirikina na washirikina ni wajibu na yule asiyeuchukia ushirikina na washirikia huyo si muislamu hata akidai uislamu na akawa anawapenda waislamu na kuipenda tauhid, lakini wapo baadhi ya waislamu ambao wanauchukia ushirikina na washirikina kwa maana wameshikamana na asili ya msingi huu lakini pamoja na hivyo wanawapenda baadhi ya washirikina au baadhi ya Mayahudi na Manaswara hukumu ya watu hawa bado ni waislamu lakini wanaupungufu wa imani zao .
Ndugu zanguni waislamu huu ndiyo uislamu lakini watu wengi leo hii hawajui maana ya uislamu kwa sababu hawajajifundisha !
Mfasiri: Ummu Muhammad
Imepitiwa na : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo mosi 24, 1445H ≈ May 3, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•