«حَسْبِيَ اللّٰهُ وَنِعْمَ الْوَكِيْلُ»
“Allah ananitosha, naye ni mbora kabisa wa kutegemewa ” .
إذا ردَّدَ العبد هٰذه الكلمَات بإخلاصٍ عند الكَرْب :
Pindi mja ataporudia rudia (kutamka) maneno haya wakati wa shida kwa moyo uliotakaswa:
نفعته نفْعاً عظيماً ، وكُنَّ له شفيعاً إلىٰ اللّٰه تعالىٰ في كِفايته شرَّ الخلْق ،
(Maneno hayo) yatamnufaisha manufaa makubwa na yatakuwa ni muombezi wake kwa Allah- aliyetukuka- katika kumlinda na shari za viumbe ,
ورَزَقَهُ من حيث لا يحتسب، وكان اللّٰه بِكُلِّ خيرٍ إليه أسرع .
Na Allah atampa riziki kwa namna asiyoitarajia, na Allah humpa haraka kila heri .
فيض القدير ؛ للمناوي:
٥ / ١٠٤
Maelezo ya mfasiri:
Haya ni matamko yenye ubora mkubwa kama ilivyothibiti katika sahihi Al-Bukhariy -Allah amrahamu-:
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ:
Kutoka kwa ibn Abbas -Allah amridhie- :
حَسْبُنَا اللَّهُ ونِعْمَ الوَكِيلُ،
“Allah ananitosha, naye ni mbora kabisa wa kutegemewa”
قالَهَا إبْرَاهِيمُ عليه السَّلَامُ حِينَ أُلْقِيَ في النَّارِ،
(Maneno) hayo aliyasema Ibrahimu -amani iwe juu yake- pindi alipotupwa motoni ,
وقالَهَا مُحَمَّدٌ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم حِينَ قالوا:
Na aliyasema Muhammad – swala na salamu za Allah ziwe juu yake- pindi (watu) waliposema :
{إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ}
“Hakika watu (yaani Makuraishi) wamekukusanyikieni kwa hivyo waogopeni” Lakini (maneno hayo) yakawazidishia imani (waislamu), wakasema: Allah anatutosha,naye ni mbora kabisa wa kutegemewa ”
آل عمران: 173
رواه البخاري .
Dua hii huombwa katika hali ya msongo wa mawazo au mfazaiko au khofu, vile vile katika hali ya shida au masaibu .
Na kwa ajili hiyo Annasaiy -Allah amrahamu- ameiwekea mlango dua hii kwa kauli yake:
” مَا يَقُول إذا خَافَ قوما “
Yale anayoyasema (muislamu) pindi atapowaogopa watu (fulani) .
من ” عمل اليوم والليلة
Kutoka kwenye kitabu chake “Amalu l-yaumi wallailah”
Na dua hii ameitaja ibn l-Qayyim -Allah amrahamu- katika :
” الفصل التاسع عشر في الذكر عند لقاء العدو ومن يخاف سلطاناً وغيره “
Kipambanuzi cha kumi na tisa katika nyiradi wakati wa kukutana na adui na (kwa) yule anayemuogopa kiongozi na wengineo .
من ” الوابل الصيب
Kutoka katika kitabu chake “Al-waabilu sswayyib”
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 28 , 1445H =May 7, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•