Acha kazi pindi muda wa swala unapofika .

كتب عمر بن عبد العزيز إلى عماله:

Umar bin Abdul- Aziz aliwaandikia wafanyakazi wake (hivi) :

«اجتنبوا الأشغال عند حضرة الصلاة

Jiepusheni na kufanya kazi pindi unapofika (muda) wa swala

فمن أضاعها فهو لما سواها من شعائر الإسلام أشد تضييعا».

Na yule aliyeipuuza/aliyeiacha hiyo (swala), basi (mtu) huyo kwa isiyokuwa hiyo swala katika nembo za uislamu ni mwenye kuzipuuza zaidi .

📚 الحلية 5/316.

Maelezo ya mfasiri:

Bila shaka swala ni nguzo ya pili katika nguzo za dini yetu ya uislamu na swala ni ibada bora zaidi inayofanywa na viungo vya mwanadamu na hiyo swala ni ya kwanza ambayo itahesabiwa siku ya kiama kama alivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:

إِنَّ أَوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ الْعَبْدُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنْ عَمَلِهِ صَلَاتُهُ

Bila shaka cha mwanzo atakacho hesabiwa nacho mja siku ya kiama katika matendo yake ni swala yake

فَإِنْ صَلُحَتْ فَقَدْ أَفْلَحَ وَأَنْجَحَ وَإِنْ فَسَدَتْ فَقَدْ خَابَ وَخَسِرَ ،

na kama (swal) itakuwa imetengemaa vizuri basi bila shaka atafaulu na atapata kile alichokitafuta (pepo), na kama (swala) itaharibika basi bila shaka ameambulia patupu (kwa kunyimwa thawabu) na amepata hasara (kwa kuadhibiwa)

فَإِنْ انْتَقَصَ مِنْ فَرِيضَتِهِ شَيْءٌ قَالَ الرَّبُّ عَزَّ وَجَلَّ :

Na kama kutapungua chochote katika swala zake za faradhi atasema Mola mlezi- akiyeshinda na kutukuka- :

انْظُرُوا هَلْ لِعَبْدِي مِنْ تَطَوُّعٍ فَيُكَمَّلَ بِهَا مَا انْتَقَصَ مِنْ الْفَرِيضَةِ ؟

Tezameni je mja wangu ana swala za suna ili kukamilishwe mapungufu yaliyopo katika faradhi ?

ثُمَّ يَكُونُ سَائِرُ عَمَلِهِ عَلَى ذَلِكَ )

kisha yatakuwa matendo yake yote hivihivi )

رواه الترمذي

Ufafanuzi wa hadithi :

Hadithi hii inaeleza kuwa cha mwanzo kitakachohesabiwa kwa mwanadamu katika haki za Allah ni swala ama kwa upande wa haki za binadamu cha mwanzo kuhesabiwa ni masuala ya kumwaga damu (kuua) , na kama swala zake za faradhi zitakuwa na mapungufu basi zitachukuliwa swala zake za suna kujazia mapungufu hayo na hili litakuwa katika kila ibada kama funga ,zaka kama kutatokea mapungufu basi kutaangaliwa suna za ibada hizo ili kuzibwa mapungufu hayo .

Na tumeona maneno ya Umar bin Abdul- Aziz -Allah amrahamu-kuwa mwenye kuipuuza swala basi mtu huyo atakuwa ni mwenye kupuuza nembo mbalimbali za uislamu yaani ibada mbalimbali kwa maana ikiwa mtu hatilii umuhimu swala basi ibada nyingine atakuwa ni mwenye kuzipuuza zaidi , na maneno haya ya Umar bin Abdul- Aziz -Allah amrahamu- yanalingana na maneno ya ibn Kathir- Allah amrahamu- katika tafsiri ya kauli yake Allah – aliyetukuka- :

۞ فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا

Lakini wakaja baada yao walio wabaya,wakapuuza swala,na wakafuata matamanio mabaya; kwa hivyo watakutana na adhabu kali .

سورة مريم (59)

akasema ibn Kathir-Allah amrahamu- pindi alipokuwa anatafsiri aya hii :

وإذا أضاعوها فهم لما سواها من الواجبات أضيع ;

Na pindi watapoipuuza hiyo (swala) basi wao kwa isiyokuwa hiyo (swala) katika mambo ya wajibu (mengine) ndiyo wenye kuyapuuza zaidi

لأنها عماد الدين وقوامه ، وخير أعمال العباد

Kwa sababu hiyo (swala) ni nguzo ya dini na nidhamu yake, na ni amali bora zaidi ya waja
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 28 , 1445H =May 7, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *