✍🏼 قال العلامة ابن القيم -رحمه الله- :
Amesema mwanawachuoni mkubwa ibn l-Qayyim-Allah amrahamu-:
قَـوله تَعـالىٰ :
Kauli yake (Allah) aliyetukuka-:
{إِذْ يَقولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّهَ مَعَنَا}.
(Mtume) alipomwambia sahibu yake : “Usihuzunike,kwa yakini Allah yu pamoja nasi”
سورة التوبة 40
فمن أصح الإشارات إشارة هذه الآية وهي :
Katika ishara zilizokuwa sahihi zaidi ni ishara ya aya hii nayo ni :
أنَّ مَن صحب الرسول ﷺ وما جاء به بقلبه وعمله وإن لم يصحبه ببدنه فإن الله معه .
Kwamba yeyote aliyeongozana na Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- na yale aliyokuja nayo kwa moyo wake na vitendo vyake ,na hata kama hakuongozana naye kwa mwili wake basi bila shaka Allah yu pamoja naye .
بدائع التفسير (٢ /١٠)
Maelezo ya mfasiri:
Maana ya maneno haya ya Sheikh-Allah amrahamu- anakusudia kuwa yeyote atakaye muamini Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie-na akamuweka moyoni mwake na akamfanya kuwa ni kiigizo chake katika matendo yake basi mtu huyo Allah atakuwa pamoja naye kwa kumpa msaada wake pale atapohitajia na atamnusuru na mabalaa mbalimbali, hii ndiyo maana ya kuongozana na Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- hata baada ya kufa kwake kwa kuongozana naye kwa moyo na kimatendo kwa kuyatekeleza yale aliyoyaamrisha na kujiepusha na yale aliyoyakataza kwa maana kufuata sunnah zake
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 29, 1445H =May 8, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•