Mapenzi yaliyokuwa matukufu zaidi !

كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .

Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :

الحبُّ الأعظم: أن تُحبُّوا الله، فأحبُّوه، وأحبُّوا ما يُحبُّه،

Mapenzi matukufu zaidi ni kumpenda Allah, basi mpendeni (Allah) na yapendeni yale anayoyapenda

وأبغضوا ما يُبغضه؛ تذوقوا حلاوة الإيمان،

na yachukieni yale anayoyachukia (mukifanya hivyo) mutaonja utamu wa imani,

فإنَّ حبَّ الله في ثلاثٍ: أن تُحبَّه، وتُحبَّ محابَّه، وتُبغضَ مباغِضَه.

na bila shaka mapenzi ya Allah yapo katika (mambo) matatu:

Kumpenda yeye (Allah), na kuyapenda anayoyapenda, na kuyachukia anayoyachukia .

الخميس 8 ذو القعدة 1445ه‍

Maelezo ya mfasiri:

Mapenzi ya kumpenda Allah ni tauhidi na ni sehemu kubwa ya ibada kwa sababu ibada ili itimie ni lazima kuwepo ndani yake mambo sita nayo ni :

1- Ukamilifu wa mapenzi ya kumpenda Allah

2-Ukamilifu wa kujidhalilisha kwake

3-Ukamilifu wa kumtukuza

4-Ukamilifu wa kumyenyekea

5- Ukamilifu wa kumuogopa

6-Ukamilifu wa kutaraji kutoka kwake .

Na makusudio ya mapenzi ya kumpenda Allah ambayo ni mapenzi ya kiibada ambayo hufuatwa na hivyo vitu sita tulivyovitaja, ni yale mapenzi ya kumpenda Allah kwa kumuabudu na kujidhalilisha kwake na kumnyenyekea mapenzi ya namna hii haifai kupelekwa kwa asiyekuwa Allah na kama mtu atayapeleka kwa asiyekuwa Allah basi atakuwa amemshirikisha Allah !.

Na pia katika kumpenda Allah tunatakiwa tuyapende yote anayoyapenda Allah kama vile kuwapenda waumini n.k ,na pia tuyachukie yote anayoyachukia Allah kama vile kuwachukia makafiri n.k, na malipo ya kutekeleza ibada hii tukufu ni kupata tamu na ladha ya imani hapa hapa duniani, utamu ambao haulingani na utamu wa chochote mpaka humfanya muumini akahisi kuwa yupo peponi kwa sababu ya ladha na utamu wa imani uliopo katika moyo wake kama alivyosema ibn Taimiyyah-Allah amrahamu- katika maneno yake mashuhuri :

…أَنَا جَنَّتِيْ وَبُسْتَانِي فِي صَدْرِيْ

“…Mimi pepo yangu na bustani langu vipo moyoni mwangu..”.

Ama mapenzi yasiyoambatana na Allah yamegawanyika sehemu nne:

1- Mapenzi ya kimaumbile kama vile mtu kupenda chakula,na kinywaji ,kulala na mengineyo ambayo ameumbiwa katika maumbile yake .

2-Mapenzi ya kutukuza na huruma na upole nayo ni yale mapenzi yaliyopo baina ya mzazi na mwanawe .

3- Mapenzi ya kuzoeana na kuchanganyika pamoja nayo ni yale mapenzi baina ya wanandoa na mtu na rafiki yake .

4- Mapenzi kwa sababu ya kufanyiwa wema wa kidunia.

Aina hizi nne za mapenzi si haramu ila pale yatakapompelekea mtu kumuasi Allah kwa kuacha kutekeleza ya wajibu au kufanya yaliyokuwa haramu .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 14, 1445H ≈ May /22, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *