✍قال الشيخ عبد الرزاق البــــــــــــدر حفظه الله :
Amesema sheikh Abdul-Rrazzaq Al-badr-Allah amuhifadhi-:
” من أهم الوسائل لتحصيل العلم النافع :
Miongoni mwa njia muhimu zaidi za kupata elimu yenye manufaa (ni):
•شغل الوقت بالتعلم والتعليم،
•ودوام المذاكرة في العلم،
Kuushughulisha wakati (wako) kwa kujifundisha na kufundisha,na kudumu (katika) kuirudiarudia na kujikumbusha elimu .
•وكثرة القراءة في الكتب النافعة،
•وتدوين الفوائد منها؛
Na wingi wa kusoma vitabu vyenye manufaa na kuziandika faida zitokazo humo,
لاسيما عند قراءة الكتب المطولة التي قد لا يتيسر للمرء أن يقرأها مرة أخرى “
Na haswa wakati wa kusoma vitabu vikubwa ambavyo huwenda mtu asipate wepesi wa kuvisoma kwa mara nyingine .
📚الفوائد المنتقاة من فتح الباري (ص9)
•••●◆❁🌸🌼🌸❁◆●•••
Maelezo ya mfasiri:
Bila shaka elimu haipatikani ila kwa kusoma kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-:
” إِنَّمَا الْعِلْمُ بِالتَّعَلُّمِ…“
“Hakika si vingine elimu (hupatikana) kwa kujifundisha ”
رواه الخطيب في تاريخ البغداد من حديث أبي هريرة -رضي الله عنه- وصححه الألباني -رحمه الله- في السلسلة الصحيحة برقم (342) .
Na kujifundisha ni:
Kuutabisha mwili, na kuwa na maazimio ya kweli, na kutakasa nia, yatakapokusanyika mambo haya matatu kwa mtu basi ataipata elimu .
Na elimu haipatikani isipokuwa kwa subira ya hali ya juu
قال يحيى بن أبي كثير -رحمه الله- :
Amesema Yahya bin Abii Kathir -Allah amrahamu-:
«لَا يُسْتَطَاعُ الْعِلْمُ بِرَاحَةِ الْجَسَدِ»،
“Elimu haiwezwi (kupatikana) kwa raha ya kiwiliwili” .
Maana yake: ili upate elimu unatakiwa ujipinde na kufanya juhudi kubwa ama ukibweteka na kupenda raha na kujitia uvivu hutopata elimu ! , na ukisoma habari mbalimbali na historia za manabii na watu wema katika hili utakutana na maajabu yenye kujulisha subira yao katika kutafuta elimu.
Allah amrahamu imamu wetu shafi aliyesema :
بقَدْرِ الكَدِّ تُكْتَسَبُ المَعَالِي
وَمَنْ طَلَبَ العُلَا سَهِرَ اللَّيَالِي
Kwa kadri ya juhudi huchumwa matukufu,na mwenye kutafuta utukufu hukesha usiku .
تَرومُ العِزَّ ثُمَّ تَنَامُ لَيْلًا
يَغُوصُ البَحْر مَنْ طَلَبَ اللَآلِي
Unakusudia (kuupata) utukufu kisha unalala usiku ,mwenye kutafuta lulu huzama baharini .
وَمَنْ رَامَ العُلَى مِنْ غَيْرِ كَدٍّ
أَضَاعَ اَلعُمْرَ فِي طَلَبِ المُحَالِ
Na mwenye kukusudia (kupata) utukufu bila ya juhudi,atapoteza umri katika kutafuta kisichowezekana .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 16, 1445H ≈ May /24, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•