NEEMA YA AMANI

رَوَى سَلَمَةُ بْنُ عُبَيْدِ اللهِ بْنِ مِحْصَنٍ الخَطْمِيِّ ، عَنْ أَبِيهِ –

Amepokea Salamah bin Ubaid -Llah bin Mihswan Al-khatmiy kutoka kwa baba yake –

وَكَانَتْ لَهُ صُحْبَةٌ –

na (huyo baba yake) alikuwa ni swahaba –

قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ :

Amesema (hivi) : Amesema Mtume wa Allah -swala na salamu za Allah zimfikie- :

(مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ آمِنًا فِي سِرْبِهِ ،

Yeyote atakayeingia asubuhi miongoni mwenu hali ni mwenye amani katika nafsi yake ,

مُعَافًى فِي جَسَدِهِ ،

Mwenye siha katika mwili wake ,

عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ ، فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا)

ana chakula cha siku mzima , basi kana kwamba amekusanyiwa dunia (yote) .

رواه البخاري في “الأدب المفرد” (رقم/٣٠٠) والترمذي في “السنن” (٢٣٤٦) وقال : حسن غريب .

Maelezo ya mfasiri:

Hapa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- anataja mambo matatu ambayo yakitimia kwa mtu basi zimethibiti kwake neema za dunia nayo ni haya :

1-Kuwa na amani  katika moyo,familia, na sehemu unayoishi .

2- Kuwa na afya katika mwili kwa kuepushwa na maradhi mbalimbali .

3- Kuruzukiwa chenye kutosha katika chakula na vinywaji .

Haya mambo matatu Allah akikuruzuku basi wewe umepewa neema ya dunia kwa sababu watu wanaitafuta dunia kwa ajili ya kupata mambo haya matatu, lakini mimi nawakumbusha ndugu zangu waislamu kuhusu neema ya amani, neema ambayo haijui thamani yake isipokuwa yule aliyeikosa kama vile katika nchi mbalimbali ambazo zinamwagika damu basi watu wake wanatamani neema hii ya amani, na bila shaka pindi amani inapokosekana basi shughuli zote za kimaendeleo zinarudi nyuma na haziendi, hakuna wageni watakaoingia kwa ajili ya biashara au mengineyo na kutokana na umuhimu wa amani ndiyo maana nabii Ibrahimu -Amani iwe juu yake- aliuombea amani mji wa  Makkah kwa sababu ni mji ambao ulikuwa hauna matunda wala mimea na kama hautokuwa na amani basi  basi hakitoletwa chochote kutoka pande mbalimbali za dunia na ikiwa hivyo basi patakuwa ni mahali ambapo watu hawatoweza kuishi ,hiyo ndiyo siri ya dua ya nabii Ibrahimu kuuombea amani mji huu pale aliposema:

{وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَذَا بَلَدًا آمِنًا..}

Na kumbuka aliposema Ibrahimu : Ee Mola wangu Mlezi !Ujaalie  huu uwe mji wa amani , ..

Sura al-baqara 126 .

Kwa umuhimu wa amani uislamu ukaharamisha kupambana na viongozi hata Kama watakuwa waovu ,kwa sababu katika kupambana nao kuna madhara makubwa ya kumwagika damu na kuondoka amani, na miongoni mwa njia za kuleta hayo machafuko na kuvunja amani ni suala la maandamano nalo pia halipo katika dini yetu ya uislamu na kama tulivyoeleza kuwa hayo maandamano ni miongoni mwa sababu za kuvunja amani .

•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Mwandishi :

Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Dhul-hijjah  (Mfungo tatu) 29, 1444H =Jun 17, 2023M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

        •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *