SIFA ZA ALIYEZAMA KATIKA ELIMU !

‏قال الإمام البغوي الشافعي – رحمه الله – :

Amesema imamu Al-Baghawiy Asshafiy -Allah amrahamu-:

‏قال الإمام البغوي الشافعي – رحمه الله – :

Amesema imamu Al-Baghawiy Asshafiy -Allah amrahamu-:

قيل الراسخ في العلم من وجد في علمه أربعة أشياء :

Kumesemwa (kuwa) aliyezama katika elimu ni yule ambaye kumepatikana katika elimu yake vitu vinne:

١. التقوى بينه وبين الله.
٢. والتواضع بينه وبين الخلق.

1-Ucha Mungu baina yake na baina ya Allah.

2-Unyenyekevu baina yake na baina ya viumbe .

٣. والزهد بينه وبين الدنيا.
٤. والمجاهدة بينه وبين نفسه.

3- Kuipa nyongo dunia baina yake na baina ya dunia

4- Kupambana na nafsi yake baina yake na baina ya nafsi yake .

معالم التنزيل 1/325

Maelezo ya mfasiri:

Hizi ndizo sifa za mwanawachuoni mwenye misingi katika elimu yake :

1- Sifa ya ucha Mungu ambayo ndiyo matunda ya elimu yenye manufaa na ucha Mungu maana yake ni kutekeleza maarisho ya Allah na kujiepusha na makatazo yake, na Allah -aliyetukuka – amewataja wanawachuoni kwa sifa hii akasema:

{ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ}

{Hakika si vingine wanaomwogopa Allah katika waja wake ni wanawachuoni}

(فاطر: ٢٨).

Kwa ajili hii imamu Ahmad -Allah amrahamu- alikuwa akisema:

أصل العِلم خشية الله

Msingi wa elimu ni kumuogopa Allah .

2- Unyenyekevu kwa viumbe pia hii ni katika sifa za wanawachuoni waliozama katika elimu, na unyenyekevu una matunda duniani au ahera au sehemu zote mbili duniani na ahera kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -:

” وما تواضعَ أحدٌ للَّهِ إلَّا رفعَهُ اللَّهُ“

“ Na hakuna yeyote aliyenyenyekea kwa ajili ya Allah isipokuwa Allah atamnyanyua”

رواه مسلم .

3- Kuipa nyongo dunia na kutosheka na kichache cha halali ni katika sifa za wanawachuoni waliozama katika elimu na kuipa nyongo dunia ni kuacha yanayomshughulisha mtu akaepukana
na ibada, hivi ndivyo walivyokuwa wanawachuoni wao waliiona dunia kuwa si chochote wakaiweka nyuma ya migongo yao :

قال أبو داود -رحمه الله- : كانت مجالسُ أحمد مجالسَ آخرة، لا يُذكر فيها شيء من أمر الدنيا، وما رأيت أحمد بن حنبل ذكر الدنيا قطّ.

Amesema Abuu Dawud- Allah amrahamu-:

Vilikuwa vikao vya Ahmad bin Hanbal ni vikao vya akhera hakutajwi chochote katika mambo ya dunia na sijapatapo kumuona Ahmad bin Hanbal akiitaja dunia katu .

4- Kupambana na nafsi pia ni katika sifa za waliozama katika elimu, kwa sababu kuna yale ambayo nafsi inayapenda lakini Allah ameyaharamisha na ili upate kufaulu mtihani huu unatakiwa upambane na nafsi yako, na bila shaka wanawachuoni wao wapo mstari wa mbele katika hili kwa sababu wao wanazifahamu aya na hadithi zilizokuja katika hili kama vile alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -amesema:

«حُفَّتِ الْجَنَّةُ بِالْمَكَارِهِ، وَحُفَّتِ النَّارُ بِالشَّهَوَاتِ»

«Pepo imezungushiwa na yale yanayochukiza na moto umezungushiwa na matamanio»

رواه مسلم.

Anasema mshairi:

والنفسُ كالطفلِ إن تهملهُ شَبَّ على ….. حُبِّ الرَّضاعِ وإنْ تَفْطِمْهُ يَنْفَطِم

Na nafsi ni kama mtoto mdogo kama utamuacha basi atakua kijana hali bado anapenda kunyonya, na kama utamuachisha ataacha .

فاصرفْ هواها وحاذرْ أنْ تُوَلِّيَهُ ….. إنَّ الهوى ما تولَّى يُصمِ أوْ يَصمِ

Basi yaondoe matamanio mabaya ya hiyo (nafsi) ,na kuwa natahadhari yasikutawale hayo (matamanio).

Hakika matamanio mabaya muda wowote yanapomtawala (mtu) humuua au humtia dosari .

Ufafanuzi wa shairi:

Mfano wa nafsi ni kama mtoto mdogo kama mama yake hatomuachisha kunyonya basi ataendelea kunyonya hata kama amefika umri ambao hatakiwi kunyonya ,na pia mtu kama ataifuatisha nafsi yake katika kufanya maovu basi siku zote atakuwa ni mtu wa kufanya maovu tu, na maradhi haya ya kufuata matamanio ya nafsi humuangamiza mtu au humtia dosari na kumfedhehesha .

Tunamuomba Allah -aliyetukuka -atustiri na kutusamehe-.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 2, 1445H ≈ Jul /8, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *