كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .
Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :
يشتدُّ على المؤمن أن ينعى أهل الإسلام، وهو يعجز عن دفع ما حلَّ بهم،
inakuwa ni uzito kwa muumini kutangaza habari ya vifo vya Waislamu na hali yeye anashindwa kuwaondolea yale yaliyowafika (katika majanga),
ويُخفِّف ألمه علمه بأنَّ الحكم لله، وهو مطلعٌ على عباده،
Na linalopunguza maumivu yake ni (kule) kujua kwake kuwa hukumu ni ya Allah pekee naye anawaona waja wake ,
ولا يُردُّ بأسه عن القوم الظَّالمين، وسوط نقمته واقعٌ بحكمته سبحانه، وله عنده أجلٌ،
Na haiepushwi adhabu yake kwa watu waovu, na mjeledi wa adhabu zake ni wenye kutokea kwa hekima zake -utakasifu ni wake – na (hilo) kwake lina muda maalumu
فيدعو بالفرج للمصابين، ويسعى بما يقدر في الدَّفع عن المنكوبين.
(anapojua hilo) basi huwaombea dua ya (kupata) faraja (wale) waliopatwa na masaibu na hufanya kila analoweza katika kuwahami wenye matatizo .
الثلاثاء ٢٠ ذو القعدة ١٤٤٥ه
Maelezo ya mfasiri:
Hii ndiyo hali ya muumini pindi anapowaona waislamu wenzake wakipata shida ni kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie:
(مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ وَتَرَاحُمِهِمْ وَتَعَاطُفِهِمْ مَثَلُ الْجَسَدِ؛ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى)
Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufanyiana kwao upole ni mfano wa mwili (mmoja) : kitapopata maumivu kiungo (kimoja) katika huo (mwili basi) mwili wote unaitana kwa kukesha na (maumivu ya) homa .
رواه البخاري ومسلم .
Kwa kweli tunaumia kwa yale yanayowapata ndugu zetu Wapalestina na tunatakiwa tukithirishe kuwaombea dua kwa Allah ndugu zetu hawa wapate nusura na awaangamize maadui wao .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 21, 1445H ≈ Jul/27, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•