كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .
Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :
يجتهد الناس في حفظ صحة قلوبهم البدنيَّة، فيتوقَّون كلَّ ما يضرُّها،
Watu wanajitahidi katika kuhifadhi siha (afya) za nyoyo zao za kimwili na wanajikinga na kila linalozidhuru (afya ya) hizo (nyoyo) ,
ويغفلون عن حفظ صحَّتها الرُّوحيَّة فلا يتوقَّون مفسدات القلوب، وأعظمها ستةٌ:
Na wanaghafilika na kuhifadhi siha (afya) yake ya kiroho na wala hawajikingi na yanayoharibu nyoyo (za kiroho), na makubwa zaidi ni (mambo) sita :
التعلق بغير الله، والاسترسال في الأمانيِّ،
1-Kushikamana na asiyekuwa Allah
2-Kuendelea kuwa na matarajio (ya kuishi muda mrefu)
وكثرة الخُلطة والكلام والنوم والطعام،
3-Na wingi wa kuchanganyika (na watu),
4- Na (wingi) wa kuzungumza,
5- Na (wingi) wa kulala,
6- Na (wingi) wa kula,
والمؤمن العاقل يتوقَّى هذا وذاك، فاحفظوا قلوبكم منها.
Na muumini mwenye akili hujiepusha na haya na yale,basi zihifadhini nyoyo zenu kutokana na hayo .
الخميس ١٥ ذو القعدة ١٤٤٥ه
Maelezo ya mfasiri :
Moyo umegawanyika sehemu mbili :
1- Kuna moyo kwa maana kipande cha nyama kilichopo upande wa kifua chako cha kushoto kwa maana ni kitu kinachoonekana .
2- Na kuna moyo wa kiroho huu ni moyo wa kimaana na huu ni ule alioutaja Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -pale aliposema:
ألا وإنَّ في الجَسَدِ مُضْغَةً، إذا صَلَحَتْ، صَلَحَ الجَسَدُ كُلُّهُ، وإذا فَسَدَتْ، فَسَدَ الجَسَدُ كُلُّهُ، ألا وهي القَلْبُ.
Sikilizeni, hakika katika mwili kuna kipande cha nyama kitakapotengemaa utatengemaa mwili (wote) na pindi utakapo fisidika utafisidika mwili (wote), sikilizeni na (kipande) hicho ni moyo .
رواه البخاري ومسلم .
Watu walio wengi hutilia umuhimu mkubwa wa kuitunza na kuihifadhi mioyo yao ya kimaumbile kutokana na vitu mbalimbali ambayo matabibu huwaambia kuwa vina madhara katika mioyo yao na tena mpaka baadhi ya watu huacha kula baadhi ya vyakula kwa kuhofia afya ya mioyo yao !.
Kinachoshangaza utawakuta watu hawa hawa hawatilii umuhimu wowote katika kuzikinga nyoyo zao za kiroho kutokana na yale yanayoharibu afya ya mioyo ya kiroho na yenye kuharibu afya ya nyoyo za kiroho ni haya sita aliyoyataja sheikh -Allah amuhifadhi- kwa maana yeyote atakayezidisha zaidi ya kiwango kinachohitajika katika haya mambo sita basi ajue atautia maradhi moyo wake kwa kupungua sehemu ya dini yake ,na mwisho sheikh akasema kuwa muumini mwenye akili ni yule mwenye kuihifadhi na kuilinda mioyo yake yote ya aina mbili : Moyo wake wa kimwili ataulinda kwa kuwasikiliza wataalamu wa afya moyo na moyo wake wa kiroho ataulinda kwa kujiepusha na haya mambo sita yenye kuharibu siha yake na pia awarejee wataalamu wa maradhi ya moyo wa kiroho nao ni wanawachuoni wa sheria na bila shaka moyo wa kiroho unatakiwa utuliwe umuhimu zaidi kwa sababu moyo huu ukipatwa na maradhi ya utata au maradhi ya matamanio movu inaweza ikawa ni sababu ya mtu kuingia Jahannam -Allah atukinge- .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 8, 1445H ≈ Aug /12, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•