كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .
Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :
(نقص الدِّين والعقل) في الرِّجال والنِّساء: آفتان تعتريان النَّفس؛ فينفلت نظامها،
Upungufu wa dini na akili kwa wanaume na wanawake ni majeraha (madonda) mawili yanayoikumba nafsi ikawa ni sababu ya kuondoka nidhamu yake (hiyo nafsi),
ويتخبط سيرها، وتختلط معاييرها،
na mwendo wa (nafsi hiyo) utakuwa ni wenye kujitupatupa ,na mizani yake ya kupima (mambo) itachanganyika
. ومن هذا النَّقص يتولَّد الفساد، وتُهتك الحرمات،
Na kwasababu ya huu upungufu huzalika ufisadi , na hufanywa yasiyoruhusiwa kufanywa,
وإذا كمُلت حصل الخير كلُّه، فتحلَوا بدينٍ صالحٍ، وعقلٍ راجحٍ.
Na pindi vitakapokamilika (viwili hivyo) kutapatikana heri zote ,basi jipambeni na dini njema na akili iliyotimia .
الأربعاء ١٠ ربيع الثاني ١٤٤٥ه
Maelezo ya mfasiri:
Upungufu wa dini na akili ni tatizo kubwa na ni sababu ya mtu kutokuwa na msimamo wa sawa na pia ni sababu ya kuleta ufisadi katika ardhi na ndiyo maana Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- pindi alipotaja sifa za Makhawariji akataja miongoni mwa sifa zao ni upungufu wa akili pale aliposema:
«سَيَخْرُجُ فِي آخِرِ الزَّمَانِ قَوْمٌ أَحْدَاثُ الأَسْنَانِ، سُفَهَاءُ الأَحْلاَمِ،
Watatokea watu zama za mwisho wenye umri mdogo, (na) wenye akili za kijinga ..
رواه مسلم .
Na bila shaka mwenye kusoma historia ya uislamu ataona namna hawa Makhawariji walivyoleta ufisadi katika kutokana na udhaifu wa imani zao na upungufu wa akili zao, na bila shaka upungufu wa dini na akili humpelekea mtu kuzungumza bila ya vipimo vya kisheria bila ya kuangalia na kuchunguza lile analolizungumza kuwa ni sahihi na kama ni sahihi je linastahiki kuzungumzwa muda huo ,na kama litazungumzwa lizungumzwe kwa sura gani kwa uwazi au kwa ishara ?
Tanbih :
Makusudio ya upungufu wa akili hapa si mtu kuwa chizi au punguani bali upungufu wa akili hapa ni kukosa maarifa ya kufikiri vizuri na kuliweka kila jambo mahali pake na kuwa na tabia ya kukurupuka katika maamuzi na hukumu n.k .
Tunamalizia kwa kumuombea Allah athibitishe imani katika nyoyo zetu na atujaalie kuwa ni watu wenye akili zilizokamilika .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 9 , 1445H ≈ Aug /13, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•