Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
๐ธุขุฏูุงุจู ุนูุดูุฑูุฉู ุงูุฒููููุฌูุฉู ููุฒูููุฌูููุง
ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.
Makala namba (9):
๐ ุฅููู ูุง ุฃูุชูุง ุงูุฒูุฌุฉ ูุฐู ุงูุขุฏุงุจ ูุฅู ุนููู ู ุซู ู ุง ุนูู ุงูุฒูุฌ ู ู ุญููู ููุงุฌุจุงุช ูุญุณู ุนุดุฑุฉ , ูู ู ุฐูู :
Chukua ewe mke hizi adabu, hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu, na kuishi kwa wema na miongoni mwa hizo (adabu ni) :
๐
ูฉ- ุงุดูุฑูู ุนูู ุงููููู ูุฅูุงู ูุชูููุฑ ุงูุนุดูุฑ ูุฅู ุตุงุญุจู ู
ุชูุนุฏ ุจุงูุณุนูุฑ ูุจุนุฏ ุงูุฎููู.
๐ธ9- Mshukuru huyo (mumeo) juu ya kichache na tahadhari na kukanusha neema za mume, hakika mwenye kufanya hivyo ni mwenye kuahidiwa adhabu na kutengwa mbali na Mwandani (wa Allah yaani Mtume) .
๐๐๐๐๐
๐ธMaelezo ya mfasiri:
๐ธSheikh – Allah amuhifadhi – anataja adabu ya tisa katika adabu za mke kuishi na mumewe, nayo ni adabu iliyokusanya mambo kadhaa :
Mosi :- Kumshukuru mume, maana yake ni hii: Mke anatakiwa amshukuru mumewe kwa ulimi wake kwa kumsifu na kwa vitendo vyake kwa kudhihirisha raha na furaha kwa kuwa pamoja na huyo mumewe, na ayasimamie mambo ya mumewe na watoto wao, na amtumikie huyo mumewe, na asimuache mumewe katika kipindi cha matatizo yaliyompata, na asiyapekue makosa ya mumewe, na amuitikie anapomuita, na ahifadhi siri zake, kwa kifupi asimshukuru mumewe kwa maneno tu lakini vitendo vyake vikawa ni vibaya kwa mumewe kwa sababu huku si kumshukuru mume, na kutomshukuru mume ni sababu ya kukasirikiwa na Allah – aliyetukuka – na kutoangaliwa kwa jicho la rahma, kama alivyosema Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie -:
๐๐๐๐๐
ูุง ููุธุฑู ุงูููู ุชุจุงุฑู ูุชุนุงูู ุฅูู ุงู ุฑุฃุฉู ูุง ุชุดููุฑู ูุฒูุฌููุง ุ ูููู ูุง ุชูุณุชูุบูู ุนููู .
“Allah – aliyezidi kheri na kutukuka – hamtizami mwanamke asiyemshukuru mumewe, na hali ya kuwa yeye hajitoshelezi bila huyo (mume) ” .
ุตุญูุญ ุงูุชุฑุบูุจ .
Pili- Mke atahadhari na tabia ya kupinga wema wa mume kwa sababu tendo hilo ni sababu ya kuingia motoni na kutengwa mbali na mwandani wa Allah [yaani Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie ], kama alivyoeleza Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – pindi alipowahutubia wanawake siku ya eid akawaambia watoe sadaka na akawaeleza kuwa yeye ameoneshwa kuwa wao ndiyo watu wengi zaidi wa motoni, na wakamuuliza :
Kwa nini ewe Mtume wa Allah? akasema:
” ุชูููุซูุฑููู ุงููููุนููู ุูู ุชูููููุฑููู ุงููุนูุดูููุฑู “
” Munakithirisha laana/matusi na munakanusha ihsani ya mume ” .
ุฑูุงู ุงูุจุฎุงุฑู .
ุฃุนุฏู :
๐ ุงูุดูุฎ ุฃูุญูู ูุฏู ุจููู ู ูุจูุงุฑููู ุจููู ููุฐูููุงูู ุงููู ูุฒูุฑูููุนููู- ุญูุธู ุงูููู-
Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy – Allah amuhifadhi .
๐๐๐๐๐
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: โ
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: โ
https://t.me/fawaidussalafiyatz
๐๏ธ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 12, 1442H โ Jul 22, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na channel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: ๐๐พ
https://t.me/fawaidussalafiyatz
โขโโโโโขโฟโโฟโขโโโโโข