Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
๐ธุขุฏูุงุจู ุนูุดูุฑูุฉู ุงูุฒููููุฌูุฉู ููุฒูููุฌูููุง
ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.
Makala namba (11):
๐ ุฅููู ูุง ุฃูุชูุง ุงูุฒูุฌุฉ ูุฐู ุงูุขุฏุงุจ ูุฅู ุนููู ู ุซู ู ุง ุนูู ุงูุฒูุฌ ู ู ุญููู ููุงุฌุจุงุช ูุญุณู ุนุดุฑุฉ , ูู ู ุฐูู :
Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :
๐
๐ธ๐ธ
ูกูก- ุทุงุนุฉ ุงููู ุณุจุจ ููุฃููุฉ ูุงููุฑุจ ููููู ุนูู ุตูุงุชู ู
ูุจูุฉ ูุนูู ุนุจุงุฏุชู ู
ุฏุงูู
ุฉ.
๐ธ11- Kumtii Allah ni sababu ya (kuleta) mshikamano na ukaribu, basi kuwa ni mwenye kuzielekea swala zako ,na mwenye kudumu na ibada zako
๐ธMaelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya kumi na moja (11) katika adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni :
kukithirisha kuswali na kudumu na ibada kwani kukithirisha kumcha Allah ni sababu ya kuimarisha na kutunza mshikamano wao baina yake na mumewe , na mwanamke ajue kuwa kukithirisha kwake kuswali na ibada mbalimbali hiyo ndiyo sababu na siri ya kuwa mrembo mbele ya mumewe ,tunaweza kusema kuwa hii ndiyo siri ya urembo bila ya kutumia mkorogo (kujichubua) , kama anavyosema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu- :
ููุฏ ูุงู ุจุนุถ ุงููุณุงุก ุชูุซุฑ ุตูุงุฉ ุงูููู ูููู ููุง ูู ุฐููุ ููุงูุช:
ุฅููุง ุชุญุณููู ุงููุฌู ูุฃูุง ุฃุญุจ ุฃู ูุญุณู ูุฌูู.
,Na kwa hakika baadhi ya wanawake walikuwa wakikithirisha kuswali usiku basi akaambiwa (mmoja wao) katika hilo, (kwa nini wafanya hivyo) akajibu: Hakika hilo hupendezesha uso na mimi napenda uso wangu upendeze.
ุงุจู ุงูููู ุฑูุถุฉ ุงูู ุญุจูู ูฃูขูก
Ufafanuzi wa maneno ya ibn l-Qayyim-Allah amrahamu:
Huu ndio urembo na uzuri halisi kwa mwanamke yaani ni dini ,na kila anapozidi kushikamana na dini urembo wake huzidi ,na haina maana kuwa mwanamke asijipambe kwa mumewe hapana ! bali kujipamba kwa mume bila ya kushikamana na dini hakuna maana .
Pili: Hawa wanawake walikuwa wakijua kuwa kisimamo cha usiku kinazipamba nyuso zao ,kama alivyosema ibn Kathir – Allah amrahamu- katika kauli yake Allah-aliyetukuka :
{ ุณููู ูุงููู ู ููู ููุฌููููููู ู ู ููู ุฃูุซูุฑู ุงูุณููุฌููุฏู }.
{ Alama zao (zipo) katika nyuso zao kutokana na athari ya kusujudu } .
Akasema ibn Kathir- Allah amrahamu-:
ููุงู ุจุนุถ ุงูุณูู: ู ู ูุซุฑุช ุตูุงุชู ุจุงูููู ุญุณู ูุฌูู ุจุงูููุงุฑ
Wamesema baadhi ya wema waliopita: ” Mwenye kukithiri swala zake za usiku uso wake hunawiri wakati wa mchana
ุชูุณูุฑ ุงููุฑุขู ุงูุนุธูู ูุงุจู ูุซูุฑ .
๐๐๐๐๐
ุฃุนุฏู :
๐ ุงูุดูุฎ ุฃูุญูู ูุฏู ุจููู ู ูุจูุงุฑููู ุจููู ููุฐูููุงูู ุงููู ูุฒูุฑูููุนููู- ุญูุธู ุงูููู-
Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .
Tarjama : Ismail Seiph Mbonde .
๐๐๐๐๐
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: โ
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: โ
https://t.me/fawaidussalafiyatz
๐๏ธ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 16, 1442H โ Jul 26, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: ๐๐พ
https://t.me/fawaidussalafiyatz
โขโโโโโขโฟโโฟโขโโโโโข