Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا
ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.
Makala namba (14):
💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :
Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :
💐
🌸🌸
١٤-لا تفتخري عليه بخلة ولا تذميه على خصلة, فاستري الذميمة وامدحي الجميلة.
🌸Usijifaharishe juu ya (mumeo) kwa jambo zuri na wala usimuaibishe juu ya jambo (baya) ,na zistiri aibu (zake)na yasifu mazuri .
🍃🍂🍃🍂🍃
Maelezo ya mfasiri:
Sheikh- Allah amuhifadhi- anataja adabu ya (14) katika adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni adabu ya kutojifaharisha juu ya mumewe, kwa jambo fulani ulilokuwa nalo ili kujiweka juu ya mumewe ,na kujitutumua juu yake mfano: akajifaharisha juu ya mumewe kwa mali alizokuwa nazo, au akajifaharisha kuwa yeye ni mzuri sana hakustahiki kuolewa na huyo mumewe ! ,bila shaka kauli hii ni haramu, au akajifaharisha kwa neema mbali mbali ambazo Allah amemneemesha ,na hukumu ya kujifaharisha ni haramu kama alivyosema Allah-aliyetukuka-:
{{ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍۢ فَخُورٍۢ }}
Hakika Allah Hampendi kila ajivunae,na ajifaharishaye .
سورة لقمان ١٨ .
Na makusudio ya kujifaharisha kuliko haramishwa hapa ni mtu kutaja neema fulani katika neema ambazo Allah amemneemesha kwa njia ya kujikweza na kujinyanyua kwa watu , na likiwa jambo hili ni haramu kumfanyia mtu yeyote bila shaka mke kumfanyia mume licha ya kuwa ni haramu bali lina madhara makubwa katika maisha ya ndoa kwa sababu litamfanya mume amuone mkewe kuwa ni mwenye kujiona na kujivuna !na mwisho wake ni ndoa kuvunjika .
Na vile vile mke anatakiwa asimlaumu mumewe juu ya aibu fulani aliyokuwa nayo bali azistiri aibu zake na ayasifu yale mazuri yake aliyokuwa nayo ,kwa maana mke awe na tabia ya kustiri makosa ya mume yale madogo madogo ambayo hakuna mtu ambaye ametakasika nayo isipokuwa Mitume , na mke anatakiwa ajue kuwa hatopata mume mwenye tabia kama za Abuu Bakr Swiddiq -Allah amridhie- kwa sababu yeye mwenyewe ucha mungu wake si kama wa Asmau bint ‘Umais- Allah amridhie- ambaye ni miongoni mwa wake wa Abuu Bakr , ikiwa hali ni hii basi ni vipi anataka mume mwenye sifa za mfano wa Abuu Bakr ? .
Na vile vile mke atambue kuwa ni lazima mumewe atakuwa na kasoro japo moja kama alivyosema Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie -:
“ كُلُّ ابْنِ آدَمَ خَطَّاءٌ وَخَيْرُ الْخَطَّائِينَ التَّوَّابُونَ ” .
” Kila binadamu ni mwenye kukosea na wabora wa wenye kukosea ni wenye kutubu” .
رواه الترمذي .
Na mshairi anasema :
وَمَن ذا الذي تُرضَى سَجَاياهُ كُلُّها !
كَفى المَرءَ نُبلاً أَنْ تُعَدَّ مَعايِبُهْ.
Na ni nani (huyo) ambaye tabia zake zote ni zenye kuridhiwa .
Inamtosha mtu kuwa na utukufu kwa kuhesabika makosa yake .
Maana ya beti hii ya shairi:
Hakuna aliyekingwa na makosa kila mwanadamu ana sehemu fulana ya makosa na mapungufu na tabia zisizoridhiwa ,lakini inatosha kwa mwanadamu kuwa mtukufu zikiwa aibu zake ni chache zinazohesabika .
🌸
🍃🍂🍃🍂🍃
أعده :
🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-
Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .
Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde .
🍃🍂🍃🍂🍃
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 23, 1442H ≈ Aug 2, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
May allah bless all of you for the good education
Maxhallah