Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا
ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.
Makala namba (16):
💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :
Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :
💐
🌸🌸
١٦- إياك والمبالغة في الغيرة فتخرجي من الممدوح إلى المذموم فيشتعل الصدر بالهموم, ويتأجج البيت بالخلافات والشكوك.
🌸16- Tahadhari na kuzidisha katika wivu ukatoka katika (wivu) mzuri na ukaingia katika (wivu) mbaya ,na kifua (moyo) kikajaa msongo wa mawazo ,na nyumba ikawaka moto kwa mizozo na shaka .
🍃🍂🍃🍂🍃
Maelezo ya mtarajumu:
Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya 16 katika adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni adabu ya kuwa na wivu wa kati na kati, kwa maana mwanamke anatakiwa awe na wivu juu ya mumewe lakini huo wivu uwe ni wivu usiochupa mipaka .
Kwa sababu wivu kwa viumbe umegawanyika sehemu mbili :
1- Wivu mzuri .
2- Wivu mbaya
Kama alivyoeleza Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- pale aliposema:
( إن من الغيرة غيرةً يحبها الله وغيرةً يبغضها الله ،
Bila shaka katika wivu kuna wivu anaoupenda Allah na kuna wivu anaouchukia Allah,
فأما الغيرةُ التي يحبها الله فهي الغيرةُ في ريبة
Ama wivu ambao Allah anaoupenda ni ule wivu katika (sehemu) yenye shaka
أما الغيرةُ التي يبغضها الله سبحانه وتعالي فهي الغيرةُ في غير ريبة ) .
Ama wivu ambao anaouchukia Allah -utakasifu ni wake na ametukuka- ni wivu katika (sehemu) isiyokuwa na shaka .
رواه أبو داود،والنسائي وأحمد وغيرهم .
Wivu unatakiwa kisheria na haswa mwanamume kwa mkewe na pia mke kwa mumewe lakini asichupe mipaka akaingia katika makosa ya kumdhania vibaya mumewe kama vile kupekua simu yake ,na wala mke asimpekue/chunguza mumewe katika kila analolifanya kwa sababu akifanya hivyo bila shaka nyumba itawaka moto yaani kutakosekana raha ya ndoa ,na wivu mbaya unatokana na udhaifu wa imani na wasiwasi wa Shetani na maradhi ya moyo ,na wivu mbaya una madhara mengi kama vile :
Kuingia katika usengenyaji,kujiingiza katika dharau,na kutomfanyia wema mume, kumdhuru, kuwafanyia uadui ndugu wa mume kutowapa haki zao,husuda,mafundo ya moyo, uchawi, kumpekua, kupata maumivu ya nafsi na mwili, kufanya hila,na vitimbi, na pengine humpelekea mtu kuua na hata huwenda ukampelekea katika makosa mengine mengi .
Ama wivu wenye sababu huo ni wivu mzuri mfano mke akamuona mumewe anaongea na mwanamke wa kando bila ya haja wala dharura, tena ni mazungumzo ambayo yanaishara mbaya, bila shaka hapa mwanamke ana haki ya kuwa na wivu kwa sababu ya hatari inayohofiwa kutokana na mazungumzo haya.
🍃🍂🍃🍂🍃
أعده :
🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-
Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .
Tarjama : Ismail Seiph Mbonde .
🍃🍂🍃🍂🍃
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 12, 1442H ≈ Jul 22, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•