ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE (17)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا

ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.

Makala namba (17):

💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :

Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :

🌸🌸
١٧- لا تخرجي إلا بإذنه ولا تصومي وتتصدقي تطوعاً إلا بعلمه.

🌸17- Usitoke (nyumbani) isipokuwa kwa idhini yake na wala usifunge (sunnah) na wala usitoe sadaka isipokuwa kwa kujua (mumeo) .

🍃🍂🍃🍂🍃

Maelezo ya mtarjumu:

Sheikh – Allah amuhifadhi- anataja adabu ya kumi na saba (17) b katika adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni adabu ya kutotoka ndani ya nyumba ila kwa idhini ya mumewe na wala asifunge funga ya sunnah na wala asitoe chochote katika mali yake isipokuwa mumewe akimrumsu, na hili la mwanamke kutotoka nyumbani ila kwa idhini ya mumewe au mlezi wake kama hajaolewa ni makubaliano ya wanachuoni wote wa fiqih, kama yalivyokuja maneno kutoka katika “Al-mausu’a l-fiqihiyyah” (19/107):

” الأصل أن النساء مأمورات بلزوم البيت ، منهيات عن الخروج … فلا يجوز لها الخروج إلا بإذنه – يعني الزوج – .

Asili kuwa wanawake ni wenye kuamrishwa kulazimiana na majumba ,ni wenye kukatazwa kutoka.. basi haifai kwa huyo (mke) kutoka ila kwa idhini yake- yaani mumewe .

قال ابن حجر الهيتمي الشافعي : وإذا اضطرت امرأة للخروج ، لزيارة والد : خرجت بإذن زوجها ، غير متبرجة .

Amesema ibn Hajar Al-haitamiy Asshaafiy : Mwanamke akipata dharula ya kutoka kwa ajili ya kumtembelea mzazi : Atatoka kwa idhini ya mumewe na (atoke) bila ya kuonesha mapambo

ونقل ابن حجر العسقلاني عن النووي عند التعليق على حديث :

Na ibn Hajar Al-‘asqalaniy amenukuu kutoka kwa Annawawiy pindi (alipokuwa anaiwekea) maelezo hadith:

( إذا استأذنكم نساؤكم بالليل إلى المسجد فأذنوا لهن )

“Pindi wanawake zenu watakapokutakeni idhini ya kwenda msikitini usiku basi wapeni idhini .

أنه قال : استدل به على أن المرأة لا تخرج من بيت زوجها إلا بإذنه ، لتوجه الأمر إلى الأزواج بالإذن “
kwamba yeye (Annawawiy) amesema : Imetumika dalili hiyo (hadithi) kuwa mwanamke asitoke nyumbani kwa mumewe ila kwa idhini yake ,kwa sababu amri ya kutoa ruhusa imeelekezwa kwao (wanamume) “.

انتهى النقل عن الموسوعة باختصار.

Na pia mwanamke haruhusiwi kufunga funga ya sunnah kama mumewe yupo ila kwa idhini ya mumewe ama zikiwa zile fungal ambazo hujirudia rudia kila mwaka kama Arafah au Ashuraa inatosha kule kutomzuia kufunga tu na wala si sharti ampe idhini,na dalili ya kutoruhusiwa kufunga fungal ya suna ila kwa idhini ya mumewe ni kauli yake Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-:

لا يحل لامرأة أن تصوم وزوجها شاهد إلا بإذنه

” Si halali kwa mwanamke kufunga (sunnah) na hali mumewe yupo ila kwa idhini yake ” .

متفق عليه .

Na vile vile mke haruhusiwi kutoa sadaka katika mali ya mumewe ila kwa idhini yake ila kikiwa ni kitu kidogo ambacho inafahamika kwa ada hiyo sehemu kuwa mume anaruhusu kitolewe, na dalili ya katazo la hili ni kauli yake Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- katika mazungumzo yake katika hija ya kuaga:

((لا تُنفِقُ امرأةٌ مِن بَيتِ زَوجِها إلَّا بإذنِ زَوجِها. قيل: يا رَسولَ اللهِ، ولا الطَّعامَ؟ قال: ذلك أفضَلُ أموالِنا )).

” Na wala mwanamke asitoe (chochote) katika nyumba ya mumewe ila kwa idhini ya mumewe .
Kukasemwa: Ewe mjumbe wa Allah, wala chakula ? akajibu: Hicho (chakula) ni bora zaidi ya mali zetu “

🍃🍂🍃🍂🍃
أعده :
🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-

Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .

Tarjama : Ismail Seiph Mbonde .
🍃🍂🍃🍂🍃
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Muharram/Mfungo nne 24, 1443H ≈ September, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *