Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا
ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.
Makala namba (18):
💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :
Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :
🌸🌸
١٨- كوني له عوناً في الحياة ومشاقها ولا تكوني عبء للحياة عليه.
🌸18- Kuwa ni msaidizi kwa (mumeo) katika maisha na mashaka yake na wala usiwe ni mzigo juu yake katika maisha .
🍃🍂🍃🍂🍃
Maelezo ya mfasiri:
Sheikh anataja adabu ya (18) katika adabu za mke kuishi na mumewe na hii ni adabu ya mwisho katika hizi adabu alizoziandaa, na adabu hiyo ni:
Mwanamke anatakiwa awe ni mwenye kumsaidia mumewe katika maisha na misukosuko yake na shida mbalimbali, na wala mke asiwe ni mzigo kwa mumewe kwa maana asimuongezee shida mumewe kutokana na maneno yake, au tabia yake au kutompa utulivu mumewe.
Mwanamke wa kiislamu anatakiwa awaige wanawake wema kama vile bibi Khadija – Allah amridhie – ambaye alikuwa ni msaidizi mkubwa wa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – na haswa pale Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – aliposhushiwa wahy na kujiwa na Malaika alirudi kwa bibi Khadija – Allah amridhie – hali ya kuwa ana hofu kwa hali iliyomtokea, basi bibi Khadija alimliwaza akamwambia maneno yafuatayo:
كَلَّا وَاللَّهِ مَا يُخْزِيكَ اللَّهُ أَبَدًا إِنَّكَ لَتَصِلُ الرَّحِمَ وَتَحْمِلُ الْكَلَّ وَتَكْسِبُ الْمَعْدُومَ وَتَقْرِي الضَّيْفَ وَتُعِينُ عَلَى نَوَائِبِ الْحَقِّ.
Hapana (usiogope) naapa kwa Allah, Allah hatokudhalilisha milele, hakika wewe unaunga udugu na unabeba majukumu ya wasiojiweza, na unawapa wale wasiokuwa nacho, na unakirimu wageni, na unasaidia mambo ya haki”
رواه البخاري .
Kwa ajili hii ndiyo maana sheikh Fauzan – Allah amuhifadhi – alipokuwa akielezea ujuzi na ufahamu wa bibi Khadija – Allah amridhie – baada ya kumliwaza Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- alisema:
وهذا من فقهها – رضي الله تعالى عنها- فهي أول من طمأن الرسول- صلى الله عليه وسلم-
Na huu ni katika ufahamu wake (bibi Khadija) -Allah aliyetukuka amridhie – na yeye ndiye wa kwanza kumtuliza Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie –
وناصره وآنسه من هذه الوحشة،
وهذا موقف عظيم منها .
na alimnusuru na kumliwaza kutokana na huu upweke na huu ni msimamo mkubwa kutoka kwa (bibi Hadija).
المصدر :
شرح ستة مواضع من السيرة.
Hivi ndivyo anavyotakiwa awe mke kwa mumewe anatakiwa ajue hali za mumewe mfano ajue kuwa : Mumewe amechoka, au amekwazwa na nini au anahitaji nini ? ,ili amsaidie katika hilo ima kwa kumfariji,au kumliwaza kwa maneno matamu mpaka akasahau shida zake ,au kumpa ushauri n.k
🍃🍂🍃🍂🍃
أعده :
🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-
Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .
Tarjama : Ismail Seiph Mbonde .
🍃🍂🍃🍂🍃
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 1, 1443H ≈ September 8, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•