ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE (NO.12)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا

ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.

Makala namba (12):

💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :

Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :

💐
🌸١٢- حياؤك وحشمتك جوهرة ثمينة فكوني في نظره دائماً جوهرة جميلة مصونة.

🌸12- Aibu yako na heshima yako ni kito /jiwe lenye thamani, basi kuwa katika mtezamo wake (mumeo) daima ni kito kizuri kinachohifadhiwa .

🍃🍂🍃🍂🍃

Maelezo ya mfasiri:

Sheikh -Allah amuhifadhi-anataja adabu ya kumi na mbili (12) katika adabu za mke kuishi na mumewe ,nayo ni adabu ya kuwa na aibu na kujiheshimu ,na akaifananisha adabu hii ni kama kito /jiwe lenye thamani lililotunzwa .
Na bila shaka mwanamke mwenye aibu na kujiheshimu hawezi akatoka nyumbani kwake bila ya dharura au haja, hawezi akayafanya yale yanayopingana na sheria ya dini.

Na aibu maana yake ni:

” Ni tabia inayopelekea mtu kufanya mema na kujiepusha na maovu/maasi ” na aibu ni tabia njema, tena ni katika tabia ambayo waislamu wanatakiwa wasifike nayo kama alivyosema Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie-:

إِنَّ لِكُلِّ دِينٍ خُلُقًا، وَخُلُقُ الْإِسْلَامِ الْحَيَاءُ

“Bila shaka kila dini inatabia na tabia ya uislamu ni haya/aibu “

صححه الألباني في “الصحيحة” (٩٤٠).

Ufafanuzi:

Yaani aibu ni tabia ambayo waislamu wanatakiwa wawe nayo na ni tabia ambayo wengi waliokuwa wema katika waislamu wanasifika nayo,

Na Mtume alikuwa ni mfano wa juu katika aibu kama anavyoelezea Said Al-Khudriy – Allah amridhie:

كان رسول الله صلى الله عليه وسلم أشدَّ حياءً مِن العذراء في خدرها . وكان إذا كره شيئًا عرفه الصَّحابة في وجهه.

” Alikuwa Mtume – swala na salamu za Allah – ana haya/aibu mno kuliko bikra katika kijumba chake. Na alikuwa anapochukia kitu Maswahaba hufahamu katika uso wake.

رواه مسلم.

Uchambuzi:

Aibu inayosemwa vizuri ni ile aibu inayomzuia mtu kufanya maovu/maasi na si aibu inayomzuia mtu kusoma dini au kuuliza, kuamrisha mema na kukataza mabaya hii si aibu! bali huu ni unyonge na uwoga,

sifa ya aibu anatakiwa kila muislamu asifike nayo lakini kwa mwanamke ni zaidi kwa sababu aibu ni kawaida ya wanawake wema tokea kale kama Allah alivyomuelezea yule binti aliyekuja kumuita Nabii Musa baada ya kuwasaidia kunywesha mifugo yao:

{ فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا ۚ }

{ Basi mmoja katika wale mabinti wawili akamjia, hali ya kuwa anatembea kwa haya/aibu. Akasema: Hakika baba yangu anakuita ili akulipe ujira wa kutunyweshea (mifugo) }

Surat Al-qas’as’: 25

Mchanganuo:

Yule mwanamke alikuja kumuita Nabii Musa hali ya kuwa ameweka mkono wa gauni lake katika uso wake kwa haya/aibu na hii pia ni dalili kuwa huo mkono wa gauni lake ulikuwa mpana kama wasemavyo wanachuoni, na hii ni dalili kuwa wanawake tokea kale walikuwa na tabia ya haya/aibu, na hii aibu na heshima kwa mke ni kama kito /jiwe lenye thamani ,na mke akisifika na tabia ya aibu na kujiheshimu huwa ni kama jiwe zuri lenye thamani lililohifadhiwa.

Ama wanawake wengi wa sasa wanaokithirisha kutoka majumbani, wanaochanganyika na wanaume sehemu mbalimbali, wanaoongea na wanaume au wanaopaza sauti katika mazungumzo yao, yote haya ni alama ya kukosa aibu.
🍃🍂🍃🍂🍃

أعده :

🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-

Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .

Mfasiri: Ismail Seiph Mbonde .
🍃🍂🍃🍂🍃
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 17, 1442H ≈ Jul 27, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *