ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE (NO.15)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا

ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.

Makala namba (15):

💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :

Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :
💐
🌸🌸
١٥- لا تبعدي عنه فينساك ولا تقربي منه فيملك وكوني قريبة لطيفة وبعيدة حبيبة.

🌸15- Usijiweke naye mbali (sana) akakusahau na wala usijisogeze karibu naye (sana) akakuchoka, (bali) kuwa karibu naye na (kuwa) mwenye huruma , na kuwa mbali naye (na hali ni) mwenye mapenzi.

🍃🍂🍃🍂🍃
Maelezo ya mfasiri:

Sheikh-Allah amuhifadhi-anataja adabu ya (15) katika adabu za mke kuishi na mumewe ,nayo ni adabu yenye kuzidisha mapenzi baina ya wanandoa nayo ni hii:

Mke anatakiwa asijiweke karibu sana na mumewe mpaka akamchoka haina maana kuwa ajitenge na mumewe kabisa isipokuwa anatakiwa awe naye karibu kidogo si kila muda kwa sababu hili hupelekea mumewe kumchoka na hapa kunadhihiri faida ya mwanamume kuwa na mke zaidi ya mmoja , na mwanamke ataona faida ya ukewenza kwa upande wake na hilo ni kwa sababu :

Pindi mwanamume anapokuwa na mke mmoja itamlazimu huyo mwanamke siku zote awe na mumewe na pia itamlazima kila siku awe amejipamba na kujiandaa kwa ajili ya mumewe lakini kama mumewe atakuwa na mke zaidi ya mmoja hilo litampa nafasi ya kupumzika baadhi ya siku yaani kile kipindi ambacho mumewe yupo kwa mke mwenzie ,na pia hiki kitendo cha kutokuwepo na mumewe kwa muda kitamuongezea hamu ya kukutana na mumewe baada ya kumkosa kwa muda!.

Na vile vile mke anatakiwa asijitenge na mumewe kiasi ambacho kikapelekea mumewe kumsahau na kumfanya mume awe katika shida na dhiki na matokeo yake ni ndoa kuvunjika .

🍃🍂🍃🍂🍃

أعده :

🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-

Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .

Tarjama : Ismail Seiph Mbonde .
🍃🍂🍃🍂🍃
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Muharram/Mfungo nne- 7, 1443H ≈ August 16, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *