ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE (NO.4)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

๐ŸŒธุขุฏูŽุงุจู ุนูุดู’ุฑูŽุฉู ุงู„ุฒู‘ูŽูˆู’ุฌูŽุฉู ู„ูุฒูŽูˆู’ุฌูู‡ูŽุง

ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.

Makala namba (4):

๐Ÿ’ ุฅู„ูŠูƒ ูŠุง ุฃูŠุชู‡ุง ุงู„ุฒูˆุฌุฉ ู‡ุฐู‡ ุงู„ุขุฏุงุจ ูุฅู† ุนู„ูŠูƒ ู…ุซู„ ู…ุง ุนู„ู‰ ุงู„ุฒูˆุฌ ู…ู† ุญู‚ูˆู‚ ูˆูˆุงุฌุจุงุช ูˆุญุณู† ุนุดุฑุฉ , ูู…ู† ุฐู„ูƒ :

Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :

๐ŸŒธ
ูค- ุฎุฏู…ุชู‡ ููŠ ุจูŠุชู‡ ุจุฌุนู„ู‡ ุฌู†ุฉ ูˆุฑุงุญุฉ ู„ุง ุชุฌุนู„ูŠู‡ ู…ู‡ุฑุจุงู‹ ูˆู…ู„ุงุฐุงู‹.
๐ŸŒธ

4- Kumtumikia (mume) nyumbani kwake kwa kuifanya (nyumba) kuwa ni bustani na (yenye) raha na wala usiifanye hiyo (nyumba) kuwa ni sehemu ya makimbilio na sehemu ya kujihifadhi /kwa muda”

Maelezo ya mfasiri:

Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya nne katika adabu za mke kuishi na mumewe ,nayo ni adabu ya kumhudumia mume na kumtumikia .

Mke anawajibika kumtumikia mumewe, na majukumu ya kuitumikia nyumba pia ni majukumu ya mke , Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie amesema :

ูƒู„ู‘ููƒู… ุฑุงุนู ูˆูƒู„ู‘ููƒู… ู…ุณุคูˆู„ูŒ ุนู† ุฑุนูŠู‘ูŽุชูู‡ ….ุŒ ูˆุงู„ู…ุฑุฃุฉู ุฑุงุนูŠุฉูŒ ุนู„ู‰ ุจูŠุชู ุจูŽุนู’ู„ูู‡ุง ูˆูˆู„ุฏูู‡ ูˆู‡ูŠ ู…ุณุคูˆู„ุฉูŒ ุนู†ู‡ู… ….ุŒ”
” Nyote ni wachunga na nyote ni wenye kuulizwa kuhusu wale aliowachunga …na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mumewe na wanae, na huyo (mwanamke) ataulizwa kuhusu hao ”

ุฑูˆุงู‡ ุงุจู† ุญุจุงู†.

Mchanganuo:

Mke kumtumikia mumewe hili ni jambo la ada na limezoeleka katika jamii mbalimbali kuwa wanawake hufanya kazi za ndani ,na ni wajibu kwake kufanya hivyo kama walivyosema baadhi ya wanachuoni -Allah awarahamu- .

Mke anatakiwa amtumikie mumewe na nyumba kwa ujumla mpaka mumewe awe anatamani kuwepo nyumbani na pindi anapokuwepo awe anahisi kama vile yupo katika bustani mzuri inayopendeza ,awe anahisi raha ,na awe anatamani kuwepo muda wote na mke asiifanye nyumba ikawa ni kama sehemu ya kukimbilia (kwa muda) au kupata hifadhi kwa muda !, na ada ya wanawake kuwatumikia waume zao ndivyo ada ya wanawake wa maswahaba,walikuwa wakiwatumikia waume zao, na wala haifai kwa mke kukataa kumtumikia mumewe ,na wala haifai kuchukua malipo maalumu kwa ajili ya huku kumtumikia mumewe , na hapa nainukuu fatwa ya sheikh Fauzan- Allah amuhifadhi- pale alipoulizwa -:

ุงู„ุณุคุงู„ ูกูฉู :

Swali la 190: ๐Ÿ“

ู‡ู„ ูŠุฌูˆุฒ ู„ู„ุฒูˆุฌุฉ ุฃุฎุฐ ุฃุฌุฑุฉ ู…ู† ุฒูˆุฌู‡ุง ุนู„ู‰ ู…ุง ุชู‡ูŠุฆู‡ ู…ู† ุงู„ุทุนุงู… ู„ุฃูƒู„ู‡ู…ุงโ€ุŸโ€

Je, anaruhusiwa mke kuchukua ujira (malipo) kutoka kwa mumewe juu ya kile chakula anachomuandalia kwa ajili ya kula?

ุงู„ุฌูˆุงุจ:

Jawabu: ๐Ÿ“š

ุงู„ู…ุฑุฃุฉ ูŠุฌุจ ุนู„ูŠู‡ุง ุฃู† ุชู‚ูˆู… ุจู…ุง ุฌุฑุช ุนุงุฏุฉ ุงู„ู†ุณุงุก ููŠ ุจู„ุฏู‡ุง ุจุนู…ู„ู‡ ููŠ ุจูŠุชู‡ุง ุจุฏูˆู† ุฃุฌุฑุฉุŒ

Mwanamke inawajibika juu yake ayatekeleze yale ambayo imejiri ada (kawaida) ya wanawake katika mji wake kwa kufanya kwao (kazi) ndani ya nyumba bila ya ujira (malipo),

ู„ุฃู† ุงู„ู…ุชุนุงุฑู ุนู„ูŠู‡ ููŠ ุงู„ุจู„ุฏ ูƒุงู„ู…ุดุฑูˆุทโ€.โ€

Kwa sababu lile lililozoeleka katika mji (fulani) ni kama liloshurutishwa.

ูˆู‚ุฏ ุฌุฑุช ุงู„ุนุงุฏุฉ ููŠ ุจู„ุงุฏู†ุง ุจู‚ูŠุงู… ุงู„ู…ุฑุฃุฉ ุจุงู„ุทุจุฎ ูˆู†ุญูˆู‡ ูู‡ูˆ ูˆุงุฌุจ ุนู„ูŠู‡ุงโ€.โ€ 

Na bila shaka yamejiri mazoea katika miji yetu (Saudia) mwanamke kusimamia kupika na mfano wa hilo basi (kazi) hiyo ni wajibu juu yake.

๐Ÿ“ ุงู„ู…ู†ุชู‚ู‰ ู…ู† ูุชุงูˆู‰ ุงู„ุดูŠุฎ ุงู„ููˆุฒุงู†.

[ Al-muntaqaa min fatawaa Sheikh Al-fauzan ]

Maelezo kutoka kwa Mfasiri – juu ya fatwa ya sheikh- Allah amuhifadhi

Mwanamke anawajibika kufanya kazi za ndani, haya ndiyo mazoea na ada sehemu mbalimbali duniani kale mpaka sasa ,hata hapa kwetu Tanzania ,na msingi wa kisheria kama alivyoeleza Sheikh unasema:

โ€ ุงู„ู…ุนุฑูˆู ุนุฑูุง ูƒุงู„ู…ุดุฑูˆุท ุดุฑุทุง โ€œ

โ€œ Kinachojulikana kwa mazoea ni kama kilichowekewa sharti โ€

Mfano ukimuoa mwanamke baada ya kumleta ndani akakwambia sipiki, sifui.. mwambie: mazoea na ada ya sehemu zetu hizi kazi za ndani ni kazi za mwanamke kwa hiyo unawajibika kuzifanya kwa maana haya mazoea ni kama sharti.

Kwa hiyo kauli inayosema kuwa mwanamke ameolewa kwa ajili ya kazi moja tu ya kumstarehesha mume! Hii kauli ni dhaifu kama alivyoeleza Sheikh Al-albaaniy – Allah amrahamu – katika “Aadaabu Zzifaaf”

Na pia tendo la ndoa wote wanalihitajia na wote wanapata raha tena kuna wanaosema kuwa mwanamke hustarehe zaidi!

Na pia wanawake wa Maswahaba walikuwa wakiwatumikia waume zao, kama vile Fatuma – Allah amridhie – alikuwa akimtumikia Aliy bin Abii Twaalib – Allah amridhie – mpaka mikono yake ikaathirika,

Hivyo tunawanasihi wanawake wawatumikie waume zao.

Na miongoni mwa sababu zilizowafanya wanawake wengi wakashindwa kuwatumukia waume zao ni kile kitendo cha kutoka majumbani mwao na kwenda kufanya kazi !na hali nyumba ni ofisi tosha ya mwanamke .

Tanbih:

Lakini ni vizuri mume kumsaidia mkewe akipata muda na huku ndiko kuishi vizuri na mke na wala si uboshoke kama wasemavyo wasio jua sheria na ndivyo alivyokuwa Mtume wetu – swala na salamu za Allah zimfikie – alikuwa akiwasaidia kazi familia yake kama ilivyokuja katika hadithi;

ู‚ุงู„ุช ุนุงุฆุดุฉ – ุฑุถูŠ ุงู„ู„ู‡ ุนู†ู‡ู…ุง:

Amesema Aisha – Allah amridhie – yeye na baba yake:

โ€ ูƒุงู† – ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู… – ูŠูƒูˆู† ููŠ ู…ู‡ู†ุฉ ุฃู‡ู„ู‡ุŒ ูุฅุฐุง ุญุถุฑุช ุงู„ุตู„ุงุฉ ุฎุฑุฌ ุฅู„ู‰ ุงู„ุตู„ุงุฉ โ€œ

โ€œ Alikuwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – anakuwa katika kuihudumikia familia yake na unapofika muda wa swala huenda kuswali โ€
๐Ÿ“š ุงู„ุจุฎุงุฑูŠ ูˆุบูŠุฑู‡.

[ Al-bukhariy na wengineo ]

Ufafanuzi wa hadithi:

Makusudio ni kuwa alikuwa Mtume – Swala na salamu za Allah zimfikie – anaisaidia familia yake kazi za nyumbani.

ุฃุนุฏู‡ :

๐Ÿ–Š ุงู„ุดูŠุฎ ุฃูŽุญู’ู…ูŽุฏู ุจู’ู†ู ู…ูุจูŽุงุฑูŽูƒู ุจู’ู†ู ู‚ูŽุฐู’ู„ูŽุงู†ูŽ ุงู„ู’ู…ูŽุฒู’ุฑููˆู’ุนููŠู‘- ุญูุธู‡ ุงู„ู„ู‘ู‡-

Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .

๐Ÿƒ๐Ÿ‚๐Ÿƒ๐Ÿ‚๐Ÿƒ

Tarjama na maelezo : fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: โ˜Ÿ
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: โ˜Ÿ
https://t.me/fawaidussalafiyatz

๐Ÿ—“๏ธ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 17, 1442H โ‰ˆ June 27, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

โ€ขโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ€ขโœฟโโœฟโ€ขโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ€ข

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *