ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE (NO.6)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا

ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.

Makala namba (6):

💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :

Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :

🌸
٦- إياك والتبذير في المال والطعام وعليك بحسن التدبيروالتقدير.

🌸6- Tahadhari na kufanya ubadhirifu katika mali na chakula na jilazimishe na upangiliaji /uendeshaja mzuri na ukadiriaji (mzuri) .

🍃🍂🍃🍂🍃

Maelezo ya mfasiri :

Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya sita katika adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni kujiepusha na kutumia mali na chakula kwa fujo ,na bila shaka uislamu umekataza ubadhirifu kwa maana utumiaji ovyo kwa fujo kama alivyosema Allah :

{… وَلاَ تُبَذِّرْ تَبْذِيراً.

Na wala usitawanye (mali yako) ovyo kwa fujo .

إِنَّ الْمُبَذرِينَ كَانُواْ إِخْوَانَ الشَّيَاطِينِ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِرَبِّهِ كَفُوراً }

Hakika wenye kutumia kwa ubadhirifu ni ndugu wa Mashetani .Na Shetani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi .

الإسراء : ٢٦-٢٧.

Na amesema Allah aliyetukuka-:

{وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ}

{Na kuleni na kunyweni .Lakini msipite kiasi .Hakika yeye (Allah) hawapendi wapitao kiasi .

[الأعراف: ٣١]

Na vilevile amesema Allah- alipokuwa akitaja sifa za waja wema :

{وَالَّذِينَ إِذَا أَنْفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَلِكَ قَوَامًا}

Na wale ambao wanapotumia hawatumia hawatumii kwa fujo ,na wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo .

الفرقان: ٦٧.

Na katika sunnah ni kauli take Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- :

كُلوا وتصدَّقوا ، والبَسوا في غيرِ إسرافٍ ولا مَخيَلةٍ

Kuleni na toeni sadaka na vaeni bila ya (kufanya) fujo wala kujigamba

رواه النسائي ٢٥٥٨ .

Mchanganuo:

Muislamu anakatazwa kufanya fujo na uharibifu katika matumizi ya mali kama vile kuvaa,kula na matumizi mengine bali anatakiwa awe mchumi yaani asiwe mbakhili na wala asitumie ovyo ,na mwanamke ambaye atakuwa na tabia ya utumiaji ovyo kwa fujo na kupita kiasi bila shaka huyu atakuwa haishi na mumewe kwa wema kwa sababu kitendo cha kuwa na tabia hii ,mke huyu hufanya ubadhirifu katika mali za mumewe ,na pia huwenda akawa ni sababu ya kumrudisha nyuma mumewe katika maendeleo kwa kule kutumia kwake ovyo mali kiwango ambacho lau angekiweka kingetumika katika matumizi mengine ,kwa hiyo matumizi ya kupita kiasi yana madhara hapa hapa duniani na pia ni haramu ,na kuna wanawake wengi wa kiislamu wanaopika vyakula vingi mpaka vikabaki na baada ya hapo hutupwa na huku ni katika kukanusha neema za Allah na sababu ya kutokea hili ni mwanamke kutokuwa mchumi na mwenye makadirio mazuri katika matumizi .

Na kuna wale ambao kila nguo wanayoiona wanaitaka ! kila mtindo utokao wa viatu au nguo yeye anataka awe nayo !,bila shaka hii ni njia ya kuingia katika utumiaji mbaya wa mali.
Ewe mke kuwa mchumi na mpangiliaji mzuri wa matumizi ya nyumbani kwako kwa kufanya kwako hivyo ni katika kuishi kwa wema na mumeo na ni sababu ya kuchangia maendeleo yake .

أعده :

🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-

Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .

🍃🍂🍃🍂🍃

Tarjama na maelezo : fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 19, 1442H ≈ June 29, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *