ADABU ZA MKE KUISHI NA MUMEWE

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا

ADABU ZA MKE KUISHI NA MUMEWE.

Makala namba (1):

💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :

Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :

١- عليك بحسن الطاعة بالمعروف ففيها ملاك الزوج ورضى الرب.

1- Jilazimishe kumtii (mumeo) kwa uzuri katika (yale) yasiyokuwa ya haramu ,basi katika huko (kumtii mume) kuna kummiliki mume na kumridhisha Mola Mlezi .

Maelezo ya mfasiri:

Adabu ya kwanza kabisa ambayo sheikh ameitaja nayo ni adabu ya wajibu kwa mke kumtekelezea mumewe ni kumtii mumewe ,na mwanamke kumtii mumewe maana yake ni mke kumtii mumewe kwa kadri ya uwezo wake bila ya kujiingiza katika kupata mashaka mazito au kujidhuru .

Na dalili ya hili kwanza kabisa katika Qurani ni kauli yake Allah -aliyetukuka- :

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَى بَعْضٍ

Wanaume ni wasimamizi wa wanawake ,kwa sababu Allah amewafadhilisha baadhi yao juu ya wengine

[النساء: ٣٤].
Ufafanuzi:

Allah ameyaweka majukumu usimamizi ni wa mwanamume kwa maana anawajibika kumsimamia mkewe kwa kumuadabisha na kumzuia ndani /asitoke ila kwa idhini yake na ni wajibu kwa mke kumtii mumewe katika yote haya maadamu hajamuamrisha la haramu .

Na dalili ya pili ni katika suna :

Kuna hadithi nyingi zinazojulisha uwajibu wa mke kumtii mume ,na katika hizo ni kauli yake Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- :

((لا يحِلُّ للمَرأةِ أن تصومَ وزَوجُها شاهِدٌ إلَّا بإذنِه، ولا تأذَنَ في بيتِه إلَّا بإذنِه، وما أنفَقَت مِن نَفَقةٍ عن غيرِ أمرِه، فإنَّه يؤدَّى إليه شَطرُه ))

“Si halali kwa mwanamke kufunga (funga ya suna) na hali ya kuwa mumewe yupo ila kwa idhini yake ,na wala asimruhusu (yeyote) kuingia nyumbani kwake isipokuwa kwa idhini yake , na (mke) hatoi kile anachokitoa bila ya amri yake (mume) , ila hakika hali ilivyo atalipwa nusu yake”

رواه البخاري .

Maana ya hadith:

Mwanamke haruhusiwi kufunga funga ya suna pindi mumewe anapokuwepo ila kwa idhini yake kwa sababu mume ana haki ya kustarehe naye muda wowote atapomuhitajia na hii ni dalili kuwa kumtii mume ni wajibu ndiyo maana kukatangulizwa juu ya ibada ya suna . Pia mke haruhusiwi kumruhusu yeyote katika kuingia nyumbani kwake ila kwa idhini ya mumewe hata akiwa ni mwanamke .Na mwanamke anapotoa sadaka kutoka katika mali ya mumewe bila ya kuamrishwa na mumewe kwa uwazi lakini akawa anafahamu kuwa mumewe hatomkataza kutoa kiwango kama hicho alichokitoa ,au ada na mazoea yanajulisha kuwa kiwango kama hicho mume hawezi kumkataza basi mwanamke huyo atapata nusu ya thawabu ,ama akitoa kiwango kikubwa bila ya idhini yake ya wazi wala kimazoea muda huo huyo mwanamke atapata madhambi .Vile vile katika faida anayoipata mke pindi atapomtii mumewe ni kummiliki huyo mumewe na kuzidi mapenzi yake kwake kwa sababu maumbile ya wanaume wanapenda kusikilizwa na kupewa nafasi yao ya utawala ktk nyumba .

أعده :

🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-

Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .

🍃🍂🍃🍂🍃

Tarjama na maelezo : fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 14, 1442H ≈ June 24, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *