ADABU ZA MKE KUISHI NA MUMEWE (N.2)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا

ADABU ZA MKE KUISHI NA MUMEWE.

Makala namba (2):

💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :

Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :

🌸
٢- القناعة كنزك في حياتك وراحة لقلبك في جميع أوقاتك.
🌸

2- Kukinai /kutosheka ni hazina katika maisha yako na ni raha ya moyo wako katika wakati wako wote.

Maelezo ya mfasiri :

Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya pili katika adabu za mke kuishi na mume nayo ni kukinai /kutosheka :

Na kukinai maana yake : Ni kuridhia kile alichokupa Allah ,na kutokodolea macho vya wengine.

Amesema Allah aliyetukuka- :

مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَى وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ

” Wale waliofanya mema,wanaume au wanawake ,hali ya kuwa ni waumini , tutawahuisha maisha mazuri ,na tutawapa ujira wao (akhera) kwa sababu ya yale mazuri waliyokuwa wakiyatenda .

(النحل: ٩٧)

Ufafanuzi : Mwenye kufanya mema atapewa maisha mazuri na baadhi ya maswahaba-Allah awaridhie wamefasiri “maisha mazuri” hapa ni kukinai/kutosheka .Rejea tafsir ya Twabariy .

Na katika sunnah kuna hadithi nyingi zinazohimiza kukinai lakini miongoni mwa hizo ni kauli yake Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- :

” قَدْ أَفْلَحَ مَن أَسْلَمَ، وَرُزِقَ كَفَافًا، وَقَنَّعَهُ اللَّهُ بما آتَاهُ “

” Bila shaka amefaulu yule aliyekuwa muislamu wa kweli ,na akaruzukiwa kinachomtosha ,na Allah akamfanya kuwa ni mwenye kutosheka kwa kile alichompa ”

رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Ufafanuzi wa hadithi :

Bila shaka muislamu wa kweli amefaulu kwa kuepukana kwake na ushirikina na ukafiri, na akapewa riziki inayomtosha isiyozidi wala kupungua akawa na uwezo wa kutatua haja zake na yale ya dharura,na Allah akamruzuku kutosheka kwa kile alichompa ambacho kinamtosha.

Na wanachuoni wengine wamesema mwenye kusifika na sifa hizo zilizotajwa katika hiyo hadithi atakuwa amepata yale anayoyataka ,na ameshinda kwa kupata anayoyataka duniani na akhera .

Ewe mke kukiwa kukinai kuna daraja hili kwa waislamu wote, bila shaka kukinai kwa mke katika maisha ya ndoa ni sababu kubwa ya kupatikana utulivu katika maisha ya ndoa kwa sababu mke asiyekuwa na tabia hii mzuri ya kukinai bila shaka atakuwa na tabia ya kukodolea vya watu na kutamani vya wengine tena vile ambavyo vipo juu ya uwezo wake !matokeo yake ni kumtia mume uzito na ikawa ndiyo sababu ya kuchukiwa na mume au kuachwa kwa sababu mke asiyekuwa na tabia ya kukinai ni mzigo usiobebeka .

Ewe mke tambua kuwa ukiwa na tabia ya kukinai na kutosheka ulichonacho basi wewe ni tajiri ,kama alivyosema swahaba mtukufu ibn Abbas- Allah amridhie-:

“القناعة مال لا نفاد له”

“Kukinai /kutosheka ni mali isiyomalizika ”

ذكره ابن عبد ربه في العقد الفريد:( ٣/١٦٩).

Kukinai kunafaida nyingi mno katika hizo ni kupata utulivu wa nafsi .

أعده :

🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-

Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .

🍃🍂🍃🍂🍃

Tarjama na maelezo : fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 15, 1442H ≈ June 25, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *