Aina za wanaume na wanawake

https://www.fawaidusalafiya.net

أنــواع الرجــال وأنــواع النســاء.

AINA ZA WANAUME NA WANAWAKE

Makala namba 01:

01 – Aina za wanawake

قـال ؏ـمر بــن الخطــاب – رضـﮯ اللـہ عنـہ

Amesema Umar bin l-Khattwaab – Allah amrahamu-:

النِّسـَاءُ ثَلاَثَةٌ: امْرَأَةٌ هَيِّنَةٌ لَيِّنَةٌ عَفِيفَةٌ مُسْلِمَةٌ وَدُودٌ وَلُودٌ تُعِينُ أَهْلَهَا عَلَى الدَّهْرِ, وَلاَ تُعِينُ الدَّهْرَ عَلَى أَهْلِهَا [ وَقَلَّ مَا تَجِدُهَا ]

Wanawake wapo sampuli tatu:

(Wa kwanza:) Mwepesi mlaini anayejizuia na machafu, muislamu, mwenye kumpenda sana mumewe, mwenye kuzaa sana, humsaidia juu ya matatizo na wala hayasaidii matatizo juu ya mumewe { Ni mara chache kumpata }

ثَانِيَةٌ: امْرَأَةٌ عَفِيفَةٌ مُسْلِمَةٌ إنَّمَا هِـﮯَ وِعَاءٌ لِلْوَلَدِ لَيْسَ عِنْدَهَا غَيْرُ ذَلِكَ.

Wa pili: Mwanamke aliyejihifadhi na machafu muislamu, hakika si vinginevyo huyo ni chombo cha (kuhifadhia) watoto na hakuna kwake isipokuwa hilo.

ثَالِثَةٌ: غُلٌّ (قيد) قَمِلٌ يَجْعَلُهَا اللَّـہُ فِـﮯ عُنُقِ مَنْ يَشَاءُ وَلاَ يَنْزِعُهَا غَيْرُهُ.

Wa tatu: Ni kitanzi cha shingo chenye chawa (kitanzi hicho) hukiweka Allah katika shingo ya amtakaye na hakuna wa kukivua isipokuwa yeye.

مصنف ابن أبـﮯ شيبة (126)

Maelezo: Hizi ndizo aina za wanawake:

1 – Mwanamke wa aina ya kwanza ni mwepesi wa tabia, ni mlaini, ni mwenye kuongozeka na kufundishika na anajihifadhi na kujitunza, mwenye kumpenda sana mumewe, mwenye kuzaa sana huwa pamoja na mumewe katika shida mbalimbali za kidunia na matatizo na wala hamzidishii mumewe matatizo juu ya matatizo na mwanamke huyu ni nadra kumpata. Ama mwenye kumzidishia mumewe matatizo ni huyu: Mfano: Mwanaume ana matatizo katika maisha na ukijumlisha na matatizo ya mdomo mchafu wa mke au tabia mbaya! inakuwa ni matatizo juu ya matatizo.

2 – Mwanamke wa aina ya pili ni yule aliyejitunza na muislamu lakini yeye hana msaada kwa mume isipokuwa kumzalia watoto tu! na huyu si mbaya lakini hamshindi wa kwanza kwa ubora.

3 – Mwanamke wa aina ya tatu huyu ni balaa tupu na ukipewa mtihani wa kuwa na mwanamke huyu ni kama vile umefungwa kitanzi chenye chawa shingoni, ukawa unapata tabu na shida ya kufungwa kitanzi hicho chenye chawa! yaani huyu ni mwanamke mwenye tabia mbaya ambaye mtu anaweza akaota mvi kabla ya uzee!balaa lake ni kubwa ndiyo maana Mmoja katika wema waliopita alikuwa akijikinga kwa Allah na mambo kadhaa na katika hayo ni aina hii ya mke! pale aliposema:

وَمِنْ زَوْجٍ تُشَيِّبُنِي قَبْلَ الْمَشِيبِ، ”

…Na (najikinga) na mke atakayenitoa mvi kabla ya (muda wa) kutoka mvi ”

… Aina za wanaume itawajia katika makala namba 02, in shaa Allah.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 26 – Rabi’ul – aakhir ≈ 11 – December – 2020M. Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM UPATE FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *