AINA ZA WATOTO NI TANO !

الشيخ محمد بن عمر بازمول -حفظه الله-

Sheikh Muhammad bin ‘Umar Baazamul- Allah amuhifadhi-:

١- أحدهم: لا يفعل ما يأمره به والداه،
فهذا ( عاقّ ) .
2- والآخر: يفعل ما يؤمر به وهو كاره ،
فهذا ( لا يؤجر ) .
3- والثالث: يفعل ما يؤمر به ، ويتبعه
بالمنّ والأذى والتأفّف ورفع الصوت
فهذا ( يؤزر ) .

1- Mmoja wao (katika hao) : Hayafanyi yale anayomuamrisha mzazi wake ,basi huyu ni mwenye kumuasi (mzazi).

2- Na mwingine :Anayafanya yale anayoamrishwa na hali ni mwenye kuchukia ,na huyu halipwi (thawabu) .

3- Na watatu : Anafanya yale anayoamrishwa ,na anayafuatishia na udhia ,na kuwaambia Ah!na kunyanyua sauti (mbele yao) ,basi huyu (mwenye tabia hii) anapata madhambi .

٤- والرابع: يفعل ما يؤمر به ، بطيبة
نفس ، فهذا ( مأجور ) ، وهم قليل .

٥- والخامس: يفعل ما يريده والداه
قبل أن يأمروا به ، فهذا هو ؛
( البارُّ الموفق ) ، وهم نادرون.

4- Na wanne: Huyafanya yale anayoamrishwa kwa moyo safi ,na huyu ni mwenye kulipwa (thawabu) ,na (wenye sifa hii) ni wachache .

5- Na watano : Huyafanya yale anayoyataka wazazi wake kabla hawajamuamrisha ,basi huyu ni mwema na aliyepewa taufiki (na Allah) ,na (wenye sifa hii) ni nadra .

🌱فالصنفان الأخيران ؛
لا تسأل عن بركة أعمارهم ، وسعة
أرزاقهم ، وانشراح صدورهم ،
وتيسير أمورهم ، و “ذلك فضل الله
يؤتيه من يشاء والله ذو الفضل
العظيم” .

Basi (watu wa) aina mbili za mwisho : Usiulize kuhusu baraka katika umri wao na wasaa wa riziki zao ,na ukunjufu (raha) ya vifua/nyoyo zao ,na kuwepesishiwa mambo yao , na “Na hiyo ni fadhila ya Allah anayompa amtakaye ;na Allah ni mwenye fadhila kubwa “

💻المصدر:صفحة الشيخ محمد بن عمر بازمول

Maelezo ya muandaaji:

Hizi ndizo aina za watoto katika kuamiliana na wazazi wao ,bila shaka makundi mawili ya mwisho ndiyo yenye kuwatendea wema wazazi wao na ktk haya mawili hili la mwisho ni kundi bora zaidi ,na kuwatendea wema wazazi ni wajibu na pia kuna matunda na faida hapa hapa duniani kabla ya akhera miongoni kwa matunda na faida ni hizo alizozitaja sheikh .

Na kuwatii wazazi wawili ni wajibu ila wakiamrisha jambo la haramu wakati huo haifai kuwatii katika hili la haramu, ila twaa katika mengine na kuwafanyia wema vinabakia pale pale na hata wakiwa hao wazazi wawili ni makafiri .

Na wema unaotakiwa kwa wazazi wawili ni kila jambo ambalo huzingatiwa kuwa ni wema katika jamii ambayo mtu huyo yupo maadamu halijakatazwa ktk sheria ,kama alivyosema Allah ,pindi alipotaja kuwafanyia wema wazazi alitaja ni wema bila ya kusema ni wema gani :

{{.. وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا}}

{Na wazazi wawili (wafanyieni) wema}}

الإسراء ٢٣ .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imesambazwa kwa mara ya pili : Mfungo Mosi 12, 1443H ≈ May 13, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *