ALIYEEPUKANA NA HAYA BASI AMEEPUKANA NA BARAKA !

❐ قال ابن القيم رحمه الله تعالىٰ :

Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:

إِن بركَةَ الرجل تَعْلِيمُه للخير حَيْثُ حلّ ونصحُهُ لكلِّ من اجْتمع بِهِ،

Hakika baraka ya mtu ni (kule) kuifundisha kwake kheri popote atapokuwepo ,na kumnasihi kwake kila aliyekusanyika naye

قَالَ الله تَعَالَىٰ إِخْبَارًا عَن الْمَسِيح :

Amesema Allah -aliyetukuka- akimuelezea Masih :

{ وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْن مَا كنت }

{ Na amenifanya ni mwenye kubarikiwa popote nilipo }

أَي : معلّمًا للخير دَاعيا إِلَىٰ الله، مذكّرًا بِهِ، مرغّبًا فِي طَاعَته،

Maana yake: (amenifanya) kuwa ni mwenye kufundisha kheri , mwenye kuwalingania (watu) wamuelekee Allah, mwenye kuwakumbusha (watu wamkumbuke) Allah, mwenye kuwapendezeshea watu twaa yake,

• فَهَذَا من بركَة الرجل، وَمن خلا من هَذَا فقد خلا من الْبركَة،

Basi haya (matendo) ni miongoni mwa baraka ya mtu ,na yule aliyeepukana na haya bila shaka ameepukana na baraka,

ومحقت بركَةُ لِقَائِه، والاجتماعِ بِهِ، بل تمحق بركَةَ من لقِيهُ وَاجْتمعَ بِهِ،

Na (pia) inafutwa baraka ya kukutana naye ,na kukusanyika naye ,bali inafutwa baraka ya yule aliyekutana na (mtu) huyo na aliyekusanyika naye,

فَإِنَّهُ يضيع الْوَقْتَ فِي الماجرياتِ
وَيفْسدُ الْقلبَ،

Basi hakika (mtu) huyo hupoteza muda katika mambo mbalimbali na huaribu moyo (wake),

• وكلُّ آفَةٍ تدخلُ علىٰ العَبْدِ فسببُها ضيَاعُ الْوَقْتِ وَفَسَادُ الْقلبِ،
Na kila maafa yanayompata mja basi sababu yake ni kupotea muda (wake) na kuharibika moyo

وتعودُ بضياعِ حَظِّهِ من اللهِ ونقصانِ دَرَجَته ومنزلتهِ عِنْدَه .

Na (hayo yote) humpotezea fungu lake litokalo kwa Allah na kupungua daraja lake na cheo chake mbele yake (Allah)

📜 رسالة ابن القيم إلىٰ أحد إخوانه(٥/١).

Maelezo ya mfasiri:

Hii ni baraka ya muislamu na makusudio ya baraka hapa ni baraka ya matendo yake mema na imani yake na miongoni mwa baraka ya matendo yake ni kule kuwafundisha kwake watu kheri popote alipo na kuwapa nasaha, na yule aliyeepukana na haya basi huyo ameepukana na baraka na pia yule anayekutana na mtu huyu hatopata baraka ya kukutana naye na kuwa naye pamoja ,kwa sababu yule ambaye ameondolewa baraka hupoteza wakati wake katika mambo yasiyokuwa na maana ,na huuaribu moyo wake kwa matendo mbalimbali .

Na kupoteza muda katika yale yasiyokuwa na faida ,na kuharibikiwa na moyo kwa kutomtaja na kumkumbuka Allah ni sababu ya kukosa mafungu ya kheri ambayo Allah amewaandalia waja wake wema na pia ni sababu ya kupungua daraja la mja mbele ya Allah.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 19, 1443H ≈ Aug 17, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *