Allah ametuumba makabila mbalimbali na rangi tofauti ili tumuabudu

قال تعالى

Amesema (Allah) aliyetukuka:

وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ سُلَالَةٍ مِنْ طِينٍ

{ Na bila shaka tumemuumba mwanadamu kutokana na udongo uliotolewa kila sehemu }

المؤمنون 12

Al-muuminuun (12)

التفسير النبوي

Tafsir ya Mtume – Swala na Salamu za Allah zimfikie –

عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال

Kutoka kwa Abii Musa Al-‘ash’ariy – Allah amridhie – kutoka kwa Mtume – Swala na Salamu za Allah ziwe juu yake – amesema:

إن الله عز وجل خلق آدم من قبضة قبضها من جميع الأرض فجاء بنو آدم على قدر الأرض جاء منهم الأبيض والأحمر والأسود وبين ذلك والخبيث والطيب والسهل والحزن وبين ذلك

Bila shaka Allah – mwenye nguvu na aliyetukuka – amemuumba Adam kutokana na gao alilolishika kutoka ardhi yote, wakaja wanadamu kwa kadri ya ardhi, Wakaja (wanadamu) miongoni mwao weupe, wekundu na weusi, na baina ya (rangi) hizo na wabaya na wazuri (kitabia) na walaini, na wagumu, na baina ya (tabia) hizo.

أخرجه أحمد والترمذي وصححه الألباني

[ Ameitoa Ahmad na Tirmidhiy na ameisahihisha Al-baaniy ] Maelezo: Kama ilivyokuwa ardhi inasifa fofauti tofauti, kuna ardhi nzuri na mbaya, kuna ardhi laini ambayo ni sifa ya mwanadamu mpole na mwenye tabia nzuri, na kuna ardhi ngumu na hii ni sifa ya mwanadamu mwenye moyo mgumu na ukatili, Na ardhi nzuri makusudio hapa ni muumini yaani muislamu wa sawa sawa ambaye huwa na manufaa matupu na ardhi ambayo ni ardhi ya chumvi makusudio ni kafiri ambaye huwa madhara matupu!

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imerudiwa kutumwa: Tarehe 10 – Safar – 1442H ≈ 27 – September – 2020M.

Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

Muhimu: Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *