ANAPOFARIKI MWANAMKE MJAMZITO MNASWARA (MKRISTO) AMBAYE MUME WAKE NI MUISLAMU NA TUMBONI MWAKE KUNA KITOTO CHA HUYO MUME .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

ANAPOFARIKI MWANAMKE MJA MZITO MNASWARA (MKRISTO) AMBAYE MUME WAKE NI MUISLAMU NA TUMBONI MWAKE KUNA KITOTO CHA HUYO MUME!

🎙 سئل شيخ الإسلام بن تيمية- رحمه الله:

“عن امرأة نصرانية, بعلها مسلم:
توفيت وفي بطنها جنين له سبعة أشهر. فهل تدفن مع المسلمين ؟ أو مع النصارى ؟

Aliulizwa sheikh -l-islam ibn Taimiyyah -Allah amrahamu:

“Kuhusiana na mwanamke wa kinaswara, na mume wake ni muislamu , akifariki na tumboni mwake kuna mtoto mwenye miezi saba, je (mwanamke huyo) atazikwa pamoja na waislamu au na manaswara?

فأجاب:

SHEIKH AKAJIBU:📚

لا تدفن في مقابر المسلمين , ولا مقابر النصارى , لأنه اجتمع مسلم وكافر ,فلا يدفن الكافر مع المسلمين, ولا مسلم مع الكافرين, بل تدفن منفردة, ويجعل ظهرها إلى القبلة؛ لأن وجه الطفل إلى ظهرها , فإذا دفنت كذلك كان وجه الصبي المسلم مستقبل القبلة, والطفل يكون مسلما بإسلام أبيه, وإن كانت أمه كافرة باتفاق العلماء”

“Hatozikwa katika makaburi ya waislamu wala makaburi ya manaswara ,kwa sababu hali ilivyo (sehemu hii) kumekusanyika muislamu na kafiri , na kafiri hazikwi pamoja na waislamu na wala muislamu hazikwi pamoja na makafiri, bali atazikwa pekeyake na mgongo wake (huyu mwanamke) utaelekezwa kibla kwasababu uso wa mtoto huelekea mgongo wake (mgongo wa mama yake) na atapozikwa hivyo (kama ilivyoelezwa) utakuwa uso wa mtoto umeelekea kibla , na mtoto anakuwa muislamu kwa uislamu wa baba yake na hata kama mama yake (ni) kafiri (na hili ni) kwa makubaliano ya wachuoni”

📚 REJEA:⇊

مجموع الفتاوى ٢٩٥/٢٤

[ Majmu’u l-fataawa: 295/24 ]

NYONGEZA YA MTARJUMU:🎙

Faida nyingine tunazopata katika fatwa hii ni hizi:⇊

1- Ufuatiliaji wa mambo uchunguzi wa hali ya juu kwa wanachuoni, tezama jinsi gani Ibn Taimiyyah amejua kuwa mtoto anaelekea upande gani anapokuwa tumboni kwa mama! pamoja na kuwa kipindi chake hakukuwa na vyombo vya uchunguzi kama katika zama zetu.

2- Pia tunapata faida kuwa pindi anapofariki mwanamke wa kikristo ambaye ni mke wa muislamu hali ya kuwa ana mimba ,huyu huzikwa sehemu iliyojitenga yaani hazikwi katika makaburi ya waislamu kwa sababu yeye ni kafiri na wala hazikwi na makafiri wenzake kwa sababu tumboni mwake kuna mtoto muislamu kwa sababu mtoto hufuata dini ya baba yake, na pia huyu mwanamke anapofukiwa hulazwa upande wake wa kushoto yaani mgongo wake huelekea kibla .

3- Maiti ya muislamu inapozikwa uso wake huelekezwa kibla.

4- Inaruhusiwa kwa muislamu kumuoa mwanamke wa kinaswara lakini kuna sharti maalum wanazozitaja wanachuoni haifai mtu kuvamiavamia, na swala hili lisizungumzwe ovyo na kila mtu bali ni kazi ya wanachuoni wetu.

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Iliandaliwa:September 18,2017M ,ikahakikiwa na kutumwa tena Shawwal 23, 1442H ≈ Jun 4, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *