Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
فإن اللسان الكذوب بمنزلة العُضو الذي قد تعطل نَفْعُه، بل هو شر منه
Basi hakika ulimi uliozoea uwongo ni kama kiungo ambacho hakina manufaa (katika mwili), bali huo (ulimi) ni wenye shari zaidi ya hicho (kiungo )
فشرُّ ما في المَرْء لِسانٌ كَذوبٌ
ولهذا يجعل اللَّه سبحانه شعارَ الكاذب عليه يوم القيامة
وشعارَ الكاذب على رسوله سَواد وجوههم
basi (kiungo) chenye shari katika mwili wa mwanadamu ni ulimi wenye tabia ya kuongopa, na kwa ajili hii Allah-utakasifu ni wake- ameweka nembo ya yule mwenye kumuongopea siku ya kiama na nembo ya mwenye kumuongopea mtume wake- (ni kuwa na) weusi (katika) nyuso zao
والكذبُ له تأثير عظيم في سواد الوجه
ويكسوه بُرْقُعًا من المقْت يراه كلُّ صادق.
na uwongo una athari kubwa katika weusi wa sura ,na humvesha (muwongo) ukaya/burqa inayotokana na kuchukiwa , na (alama) hiyo huiona kila mkweli .
إعلام الموقعين ( ٢/٢٣٥ )
Maelezo ya mfasiri:
Mtu mwenye ulimi wenye sifa ya uwongo ni kama yule mwenye kiungo kilichopooza kisichokuwa na kazi na manufaa yoyote katika mwili, bali ulimi wenye sifa ya uwongo shari yake ni kubwa zaidi kuliko kiungo hicho kilichopooza na kisichokuwa na manufaa yoyote !.
Mtu muwongo ni mwenye kudhalilika duniani na akhera ,na Allah -aliyetukuka- ameweka alama na nembo katika sura zao zinazojulisha kuwa hawa ni waongo , ama siku siku ya kiama waongo wale waliomuongopea Allah na kumzushia uwongo kama vile wale waliodai kuwa Allah ana mtoto au ana washirika watakuwa na weusi katika nyuso zao ,amesema Allah:
{وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ تَرَى الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَى اللَّهِ وُجُوهُهُمْ مُسْوَدَّةٌ }
Na siku ya kiama utawaona wale waliomsingizia uwongo Allah nyuso zao zimekuwa nyeusi .
الزمر ( ٦٠) .
Na ibn l-Qayyim- Allah amrahamu- anasema kuwa uwongo huleta athari ya weusi wa uso kwa maana mtu mwenye tabia ya uwongo huwa na weusi usoni mwake lakini weusi huu hauonekani kwa kila mtu bali huuona kila muumini mkweli na alama hii ya weusi katika uso wa mtu muwongo huwa kama ukaya /niqabu aliyoivaa katika uso wake ,na pia mtu muwongo huchukiwa na kubughudhiwa.
Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 19, 1443H ≈ September 26, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•