ATHARI YA MWANAMKE KATIKA MAISHA YA MUMEWE !

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

ATHARI YA MWANAMKE KATIKA MAISHA YA MUMEWE

Makala no: 04

Kutoka kwa shekh Muqbilu bin Hadiy – Allah amrehemu

فإن النبي صلى الله عليه وعلى آله وسلم يقول كما في ( الصحيحين ) من حديث أبي موسى الأشعري رضي الله عنه : ” مثل الجليس الصالح ، وجليس السوء ، كحامل المسك ونافخ الكير ، فحامل المسك إما أن تبتاع منه ، وإما أن يحذيك ، وإما أن تجد منه ريحاً طيبة ، ونافخ الكير إما أن يحرق ثيابك ، وإما أن تجد منه ريحاً منتنة “.

Kwa hakika Mtume – swala na salam za Allah ziwe juu yake – anasema (kama ilivyokuja) katika sahihi mbili katika hadithi ya Abu Musa Al-ashaa’riy – Allah amridhie-:

“Mfano wa rafiki mwema na rafiki muovu, ni kama mbeba (muuza) miski na fundi mhunzi, basi mbeba miski ima ununue kutoka kwake (hiyo miski) na ima akupe na ima upate kutoka kwake harufu nzuri, na fundi mhunzi ima akuunguzie nguo zako, ima upate kutoka kwake harufu mbaya “.

فأنصح كل أخت ، كما أنني أنصح كل أخ أن يتحرى ، خصوصاً النساء فإنهن ضعيفات ، والرسول صلى الله عليه وعلى آله وسلم يقول كما في ( الصحيحين ): “استوصوا بالنساء خيراً فإنهن خلقن من ضلع ، وإن أعوج ما في الضلع أعلاه ، فإن ذهبت تقيمه كسرته ، وإن تركته لم يزل به عوج ” ، فالمرأة ضعيفة ربما يفتنها الرجل ، لا أقول: ربما بل قد حدث ، أنصح المرأة الصالحة إذا أراد أبوها الجشع أن يزوجها بـرجل من أهل الدنيا أن تقول: هى لا ترغب في الزواج حتى يأتيها رجل صالح ، وتتزوج بالرجل الصالح ، وقد تكلمنا على هذا في ( المخرج من الفتنة ).

Basi na muusia kila dada, kama ninavyomuusia kila kaka kutafuta (kupekua), hasa wanawake bila shaka wao ni wenye udhaifu wa nafsi, na Mtume swala na salamu za Allah ziwe juu yake anasema kama (ilivyokuja) katika sahihi mbili:

“Wafanyieni wema wanawake hakika hao wameumbwa kwa ubavu na hakika sehemu iliyopinda zaidi katika ubavu ni (ile) ya juu yake, ukitaka kuunyoosha utauvunja na ukiuacha utauacha (hali) ya kuwa ni wenye kuendelea kupinda”.

Mwanamke ni dhaifu huenda akafitinishwa na mwanaume, sisemi huwenda bali hakika (hili) limetokea, na muusia mwanamke mwema pindi baba yake mwenye uroho wa mali atakapotaka kumuozesha kwa mwanaume katika watu wa dunia (wenye mali), aseme (kuwa): Yeye hapendi kuolewa, mpaka atakapomjia mume mwema, na aolewe na mtu mwema, na hakika tumelizungumza hili katika (muhadhara wa) [Al-makhraji minal-fitnah ]

🔦 من شريط: (أسئلة نساء تعـــز: اليمن)

Kutoka katika kaseti (Maswali ya wanawake wa Ta’az -Yaman)

🔈 للإستماع للصوتية:

Kwa kusikikiza sauti (bonyeza hapa)

Maelezo:

Hivi ndivyo rafiki anavyomuathiri yule anayehusubiana naye kama tulivyoona katika hiyo hadithi bali katika kuambatana na mtu mwema kuna faida nyingi hata kama hukuchuma kwake wema wowote kule kuepukana na shari tu ni wema tosha, na bila shaka wanandoa wanaathiriana zaidi katika maisha yao !

Inaendelea –

✍️ Usikose sehemu inayofuata katika nasaha za Sheikh Allah amrehemu …

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 10, 1442H ≈ May 22, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

DARSA ZA NDOA INGIA HAPA: ⤵️
https://t.me/Darasazandoa

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *