https://t.me/fawaidussalafiyatz Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
ATHARI YA MWANAMKE KATIKA MAISHA YA MUMEWE
Makala no: 05
Kutoka kwa shekh Muqbilu bin Hadiy – Allah amrehemu
وكذلك المرأة الفاسدة ربما تفسد زوجها ، فقد عرفت رجلاً صالحاً فاضلاً زارنا إلى هنا من بلد من أرض الله الواسعة ، وبعدها فما شعرنا إلا وقد تغيرت أحواله ، وعرف إخوانه أن فساده بسبب امرأته ، فجزى الله إخوانه خيراً ، أخذوها على سيارة معه وذهبوا بها إلى أهلها حتى لا تفسد ذلك الرجل الصالح ، ثم ردها ورجع على ما هو عليه – انقلب على ما هو عليه – والآن أخبرت أنه فارقها ورجع إلى الخير والصلاح .
Na vilevile mwanamke muovu huwenda akamharibu mumewe, hakika namjua mtu mwema mbora alitutembelea hapa kutoka katika mji (fulani) katika ardhi ya Allah iliyokuwa pana, na baadae, ghafla tukahisi kubadilika hali yake, na wakatambua ndugu zake kwamba kuharibika kwake ni kwa sababu ya mkewe – Allah awalipe kheri ndugu zake – walimchukua mwanamke na kumtia kwenye gari pamoja na mumewe wakaenda naye kwao ili asije akamharibu yule mtu mwema, kisha wakamrudisha huyo (mwanamke kwao), na (yule mwanaume) akarudi kama alivyokuwa nayo, akabadilika (akawa) kama alivyokuwa (zamani), na hivi sasa nimepewa khabari kwamba ameachana naye na (huyo mwanaume) amerudi katika kheri na wema.
🔦 من شريط: (أسئلة نساء تعـــز: اليمن) Kutoka katika kaseti (Maswali ya wanawake wa Ta’az -Yaman) 🔈 للإستماع للصوتية:
Kwa kusikikiza sauti (bonyeza hapa) https://muqbel.net/files/fatwa/muqbel-fatwa1083.mp3
Maelezo ya mfasiri: Katika kisa hiki tumejifunza kuwa waweza ambatana na mtu muovu kwa lengo la kumuweka sawa akakuingiza wewe katika uovu wake! Nasaha kwa wale wanaooa wanawake waovu kwa kuvutiwa na sura au umbo na kusema nitamuweka katika msimamo, Watu hawa waziogopee nafsi zao wasije wakavutwa wao katika uovu bali wazingatie muongozo wa – Mtume swala na salamu za Allah ziwe juu yake – katika kutafuta mchumba.
Inaendelea –
✍️ Usikose sehemu inayofuata katika nasaha za Sheikh Allah amrehemu … Muandaaji: fawaidusalafiya.net Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 13, 1442H ≈ May 25, 2021M. #Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
DARSA ZA NDOA INGIA HAPA: ⤵️ https://t.me/Darasazandoa Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•