CHOZI LA HUZUNI JUU YA TAUHID NA AQIDAH !

كتب شيخنا إبراهيم المحيميد -حفظه الله- عبر حسابه على تويتر :

Ameandika sheikh wetu Ibrahimu Al-Muhaimid -Allah amuhifadhi – kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :

لو ظهر الدجال وزعم أنه الرب وتبعه الخلائق لا يستغرب.

Lau angedhihiri (Masihi) wa uwongo ,na akadai kuwa yeye ndiye Mola na viumbe wangemfuata (hilo) halitoonekana geni .

كافرة ما سجدت لله سجدة وعقيدتها أن عيسى ابن الله كشفت حقيقة تدين الناس ،

Mwanamke kafiri (ambaye) hajapatapo kumsujudia Allah hata sijida moja na itikadi yake kuwa Isa ni mtoto wa Allah (huyu mwanamke) amefichua uhakika wa dini ya watu ,

البعض صلى عليها صلاة الغائب ،والبعض اعتمر عنها والبعض حكم لها بالشهادة .

Kuna baadhi waliomswalia swala ya mbali ,na kuna baadhi waliomfanyia (ibada) ya umrah,na kuna baadhi wamempa hukumu ya (kuwa ni) shahidi.

رسالتي لأهل السنة:

قُلْ بِفَضْلِ ٱللَّهِ وَبِرَحْمَتِهِۦ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُواْ

Ujumbe wangu kwa Ahlu sunnah :

{Sema : “Kwa fadhila za Allah na kwa rehema zake ” Basi na wafurahi kwa hayo.

Imeandika tarehe 13/Shawwal/1443 H.

Maelezo ya mfasiri :

Sheikh -Allah amuhifadhi ameandika maneno haya
baada ya kuuawa kwa mwandishi wa habari wa al-Jazeera, Shireen Abu Akleh, aliyepigwa risasi imedhihiri kuwa waislamu wengi zaidi hawafahamu aqidah (itikadi) yao sahihi na Tauhid kwa sababu kuna wengi walio mtakia msamaha, na kumuita shahidi, bali kuna wale waliomswalia swala ya mbali na kuna wale walioenda kumfanyia ibada ya Umrah! na hali mwandishi huyu alikuwa ni kafiri! , na zipo dalili nyingi na yamepita makubaliano ya Maulamaa juu ya uharamu wa kumtakia msamaha kafiri!, lakini hili linajulisha namna wengi zaidi katika waislamu hawaifahamu dini yao.

Na ndani yake kuna mahimizo ya kuwa tuzidishe juhudi katika kusoma na kufundisha aqidah na tauhid.

Pia sheikh mwishoni akawaambia Ahlu sunnah wafurahi kwa neema hii ya Uislamu na Sunnah, neema ya kushikamana na uislamu halisi aliokuja nao Mtume -Swala na salamu za Allah zimfikie -na bila shaka Ahlu sunnah ndiyo wenye kuifahamu itikadi halisi na wao hawawezi kuingia katika makosa makubwa kama haya ya kiitikadi.

Tanbih : Uislamu unapinga dhulma kwa kila mtu kwa ajili hiyo tunasema kuwa huyu mwandishi wa habari ameuliwa kwa dhulma na hawa madhalimu wa Kiyahudi ,lakini hili halipelekei tukampa hukumu ya kuwa yeye ni muislamu kama walivyofanya hao wasiojitambua.

Mwisho : Waislamu wajue kuwa kuuawa huyu mwanamke ni kosa lakini hakuna kosa kubwa zaidi ya kumkufuru Allah na kumshirikisha Allah, na huyu mwanamke amekufa hali amemkufuru Allah.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo mosi 16, 1443H ≈ May 17, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *