عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنَّ رَجُلًا أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ:
Kutoka kwa ibn Umar kuna mtu alimjia Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- akasema:
يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي أَصَبْتُ ذَنْبًا عَظِيمًا فَهَلْ لِي تَوْبَةٌ ؟
Ewe Mtume wa Allah , hakika mimi nimefanya dhambi kubwa je nina (nafasi) ya toba ?
قَالَ: (هَلْ لَكَ مِنْ أُمٍّ؟)
(Mtume) akasema: Je una mama ?
قَالَ: لَا، قَالَ: (هَلْ لَكَ مِنْ خَالَةٍ؟) قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: (فَبِرَّهَا).
(Yule mtu) akasema: Hapana, (Mtume) akasema (tena): Je una mama mdogo/mkubwa ? , akasema: Ndio , (Mtume) akasema : Basi mfanyie wema huyo.
رواه الترمذي (١٩٠٤) صححه الألباني في “صحيح الترغيب” (٢٥٠٤)
Maelezo ya mfasiri:
Hii hadithi inajulisha kuwa kumfanyia wema mama mdogo/mkubwa ni katika matendo bora na ni katika matendo yanayofuta madhambi .
Mama mdogo ana nafasi tukufu katika uislamu na ana daraja la mama mzazi kama ilivyothibiti katika hadithi nyingine.
عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عن رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أنّه قَالَ : ( الْخَالَةُ بِمَنْزِلَةِ الْأُمِّ )
Kutoka kwa Aliy -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- kuwa yeye amesema:
{Mama mdogo ana daraja la mama }
رواه أبو داود (٢٢٧٨) وصححه الألباني في “صحيح أبي داود” .
قال الذهبي -رحمه الله- في ” الكبائر” :
Amesema Addhahbiy -Allah amrahamu-:
“أي : في البر والإكرام والصلة”
Maana yake: (ana daraja la mama mzazi) katika kufanyiwa wema na kukirimiwa na kuungwa .
Tanbih:
Mama mdogo au mama mkubwa ni yule ndugu wa mama yako mzazi yaani mdogo wake au dada yake ,na pia mama mdogo wa mama yako au baba yako hao pia ni mama zako wadogo .
Na mama mdogo ni katika maharimu wa mtu yaani mtu anaruhusiwa kumpa mkono ,na kusafiri naye na kukaa wawili pamoja bila ya yeyote na pia mama mdogo anaruhusiwa kupunguza hijabu mbele yake.
Kusahihisha ufahamu:
Mke wa baba yako mdogo au mkubwa huyo si mama mdogo ,na wala mke wa mjomba wako si shangazi yako na ndiyo maana katika sheria kama baba yako mdogo au mkubwa akifariki au akimuacha mkewe na eda ikamalizika unaruhusiwa kumuoa mkewe na pia mke wa mjomba .
Mfasiri :Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 7, 1443H ≈ Jan,10 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•