كتب الشيخ عبد العزيز الشايع -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .
Ameandika sheikh Abdul-Aziz Asshayi’i -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :
العلم ثلاثة أشبار:
Elimu ni shibiri tatu :
١-من دخل الأول تكبر
٢-ومن دخل الثاني تواضع
٣-ومن دخل الثالث علم أنه مايعلم
1-Yule aliyeingia (shibiri) ya kwanza hutakabari (huwa na kiburi) .
2-Na yule aliyeingia (shibiri) ya pili hunyenyekea.
3-Na aliyeingia (shibiri) ya tatu hujua kuwa yeye hajui.
البعض يطول به الزمن في الشبر الأول
Baadhi (ya watu) hurefukiwa na muda katika (hiyo) shibiri ya kwanza.
ولا يصل للثاني إلا موفق
ولا يدرك الثالث إلا عالم راسخ
Na hakuna anayefika (shibiri) ya pili ila yule aliyewafikishwa (na Allah), na wala hafiki (shibiri) ya tatu ila ni mwanachuoni aliyebobea.
قال الزهري:
Amesema Zuhriy :
طلبت العلم حتى ظننت أني اكتفيت، فلما لقيت عبيدالله بن عتبة علمت أنه ليس عندي شيء
Nilitafuta elimu mpaka nikadhania kuwa nimetosheka, basi pindi nilipokutana na Ubaidullah bin ‘Utbah nikajua kuwa mimi sina chochote katika elimu.
Jun 25, 2019
Maelezo ya mfasiri :
Hizo ndizo daraja za elimu yaani ni shibiri tatu :
Na shibiri ni umbali mkubwa kati ya kidole gumba na kidole cha mwisho kwenye mkono mmoja, na kama alivyoeleza sheikh – Allah amuhifadhi – watu wengi hubakia katika shibiri ya kwanza kwa muda mrefu pengine maisha yao yote hubakia hapo hapo mpaka kifo kinawafika na hawa ndiyo watu wenye kiburi kwa kujiona kuwa wanajua kumbe hawajui!
Ama atakayeingia shibiri ya pili huwa na unyenyekevu kwa sababu yeye anajua kuwa kile anachokifahamu ni kichache mno.
Ama mwenye kuingia katika shibiri ya tatu kutoka na kusoma kwake na kubobea katika elimu, hutambua kuwa elimu ni bahari isiyokuwa na ufukwe na kile anachokijua yeye si chochote katika elimu kana kwamba hajui chochote, na wanaofika katika shibiri hii ya tatu ni wachache mno ambao Allah amewapa taufiki hiyo.
Tunamuomba Allah atupe elimu yenye manufaa.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 18, 1445H ≈ Nov 3, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•