Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
قـال الشيخ عبد الرزاق بن عبد المحسن البدر – حفظه الله:
Amesema Sheikh Abdul-Rrazzaaq bin Abdil-Muhsin Al-badr – Allah amuhifadhi:
ومن الأمور المؤسفة أنّ كثير من النّساء لا تعرف الزّينة و التّجمّل،
Katika mambo yanayosikitisha kwamba wengi katika wanawake hawatambui (kutumia) mapambo na kujiremba,
إلا إذا أرادت أن تخرج من البيت،
ila (hujiremba) pindi anapotaka kutoka nyumbani,
و تغادره لحضور مناسبة أو اجتماع أو ما نحو ذلك،
Na (anapotaka) kuiacha (nyumba) kwa ajili ya kuhudhuria mnasaba (fulani) au mkusanyiko (fulani) au mfano wa (mambo) hayo,
أمّا فيما يتعلّق بحقّ الزوج،
Ama katika yale yanayohusiana na haki za mume,
إذا دخل فتلقاه بثياب رثّة،
Pindi atakapoingia (mume ndani) humkuta na nguo za ovyo ovyo,
وبرائحة غير طيّبة،
Na harufu isiyokuwa nzuri,
وبشعرٍ شعث،
Na nywele timutimu,
وبصفات تصدّه عنها،
Au (humkuta akiwa) na sifa zinazomzuwia na (kumkaribia),
وتقطع من رغبته فيها،
Na zinakata matamanio yake kwa huyo (mkewe),
فأيّ رغبة تملأ قلب هذا الزوج،
Basi ni mapenzi gani yatakayoujaza moyo wa huyu mume,
تجاه من هذه صفاتها ؟
Kwa upande wa (mwanamke ambaye) sifa zake ni hizi ?
وأيّ حبّ يكتنف جوانحه إذا كان هذا شأنها معه ؟
Na mapenzi gani yatakayochota pande zake(mwanamume huyu) ikiwa hii ndiyo hali yake (mwanamke huyu) pamoja na huyo (mumewe) ?
وهذا مـن دلائـل حمــق المــرأة،
Na hii ni katika alama za upumbavu wa mwanamke (huyu),
وقلّــة عقلِهــا في تحقيق كمال الحياة الزوجية،
Na uchache wa akili yake katika kuthibitisha vizuri ukamilifu wa maisha ya ndoa,
وتحقيق سموّها ورفعتِها.
(Na uchache wa) kuuthibitisha vizuri utukufu (wa ndoa) na ule ubora wake.
📚 من كتاب صفات الزوجة الصالحة (صـفحة ٢٤)
Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi
Mke kutojipamba na kujiremba kwa ajili ya mumewe hili ni kosa kubwa tena husababisha ndoa kuyumba yumba au kuvunjika kabisa kwa sababu mume hapati hamu ya kukutana na mkewe, ndiyo maana sheria ikaweka ni suna mwanamke kujipamba ili mume anapomuona apate hamu ya kumuingilia na inakuwa ndiyo sababu ya ummah kuongezeka,
Kwa hiyo mke anatakiwa ajipambe na kujiweka vizuri mpaka mume akimuona tu apate raghbah na tamaa kwa kule kuvutiwa na mkewe kwa jinsi alivyojirembe na kupendeza…
Pengine baadhi ya wanaume wakaenda kuongeza mke mwingine kwa sababu ya kuona mapungufu haya! akawa akiingia ndani kila siku anamuona mkewe katika hali ya ovyo ovyo!
Tanbihi: Mwanamke anapojipamba akatoka nje ya nyumba na kuonesha mapambo yake na viungo vyake vya mwili kwa wanaume wa kando (wanaume wanaoruhusiwa kumuoa) mwanamke huyo anapata madhambi.
Mtarjumu: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy.
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Toleo la pili: Mfungo sita 30, 1443H ≈November 5, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•