FAIDA KUTOKA KATIKA QURAN

۞ قال الله تعالى :

Amesema Allah -aliyetukuka-:

    ﴿ إِذْ أَوَىٰ الْفِتْيَةُ إِلَىٰ الْكَهْفِ ﴾

{ Pindi vijana walipokimbilia katika pango }

قال العلَّامة عبد الرحمٰن السعدي رحمه الله:

Amesema mwanachuoni mkubwa Abdul-Rrahman Assa’adiy-Allah amrahamu-:

• في هذه القصة دليل علىٰ أن من فر بدينه من الفتن، سلمه الله منها .

Katika hiki kisa kuna dalili kuwa yule atakayekimbia na dini yake kutokana na fitna Allah atamsalimisha na hizo (fitna)

• وأنّ من حرص علىٰ العافية عافاه الله ومن أوىٰ إلىٰ الله، آواه الله، وجعله هداية لغيره،

Na kwamba mwenye kupupia juu ya ulinzi Allah atamlinda,na mwenye kukimbilia kwa Allah, Allah atamuhifadhi na atamfanya ni (sababu) ya kuongoka wengine,

• ومن تحمل الذل في سبيله وابتغاء مرضاته،
كان آخـر أمره وعاقبته العز العظيم من حـيث
لا يحـتـسـب

Na mwenye kuvumilia udhalili katika njia yake (Allah) na (katika) kutafuta radhi zake,mwisho wa jambo lake na ukomo wake utakuwa ni utukufu mkubwa kwa upande asiotarajia.

{ وَمَـا عِـندَ اللَّـهِ خَـيْـرٌ لِّلْأَبْـــرَارِ }.

Na vilivyoko kwa Allah ni bora kabisa kwa watu wema

📕[ تيسير الكريم الرحمٰن: (٤٧٣/١)

Maelezo ya mtarjumu:

Sheikh-Allah amrahamu- anataja katika faida zinazopatikana katika kisa cha vijana wa pangoni ni kuwa kama mtu atakimbilia kwa Allah kwa kujikinga na fitna basi Allah atamlinda na fitna, na mwenye kuvumilia na kusubiri pamoja na kudhalilika kwa ajili ya dini basi mwisho wake Allah atampa utukufu !

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 9 , 1443H ≈ Feb 10, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *