Makala namba (12) .
قال شيخ الإسلام ابن تيمية رحمه الله:
Amesema sheikh l-Islam ibn Taimiyyah -Allah amrahamu -:
• من كان الله معه دفع عنه أنواع الأذى والمضرات مالا يدفعه عنه أحد من خلقه، قال تعالى:
Yule ambaye Allah yu pamoja naye humuondolea aina za maudhi na madhara (uondoaji) ambao hawezi kumuondolea yeyote katika viumbe ,amesema (Allah) aliyetukuka :
{ وَاصْبِرُوا ۚ إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ}
{Na subirini . Bila shaka Allah yu pamoja na wenye kusubiri }.
وقال تعالى:
{ وَاللَّهُ يُحِبُّ الصَّابِرِينَ}
Na amesema (Allah) aliyetukuka -:
{Na Allah anawapenda wenye kusubiri}
📚 جامع المسائل جـ١صـ١٧٢.
Maelezo ya mfasiri :
Allah yu pamoja na wafanyao subira na kuvumilia kwa maana huwasaidia na kuwakinga, kuwapa nguvu juu ya maadui zao n.k , na Allah huwapenda wale wafanyao subira ambao huwa na subira katika yale ambayo wameamrishwa wawe na subira, na subira imegawanyika sehemu tatu:
1-Kuwa na subira juu ya kumtii Allah kwa maana mja asijisikie dhiki katika kufanya ibada na asiache.
2- Kuwa na subira katika kuyaacha maovu kwa maana asiyafanye maovu.
3- Kuwa na subira juu ya makadirio ya Allah yenye kuumiza kwa maana anatakiwa mtu asikasirike kwa sababu ya yale ambayo Allah ameyakadiria juu yake katika kadari zenye kuumiza kwake kama vile maradhi,njaa,n.k
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shabani 22, 1443H ≈ Mar 25, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•