Makala namba (2)
قال الله تعالى :
Amesema Allah aliyetukuka-:
{وَاللهُ لا يَهْدِي القوْمَ الظّالِمينَ}
{Na Allah hawaongozi watu madhalimu}
البقرة: ٢٥٨.
▪️قال العلامة ابن عثيمين -رحمه الله-:
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn ‘Uthaimin -Allah amrahamu-:
“فإذا كان الظالم لا يهديه الله، فصاحِب العدل حري بأن يهديه الله عز وجل،
Basi akiwa mtu dhalimu Allah hamuongozi basi mwenye uadilifu anastahili kuongozwa na Allah-aliyeshinda na kutukuka-
فإن الإنسان الذي يريد الحق ويتبع الحق، والحق هو: العدل، غالبًا يُهدى، ويُوَفّق للهداية”.
Hakika mwanadamu ambaye anaitaka haki na anaifuata haki, na haki ndiyo huo uadilifu (mtu huyu) aghlabu huongozwa na hupewa taufiki ya kuongoka.
ولهذا قال شيخ الإسلام ابن تيمية في العقيدة الواسطية عبارة من إحسن العبارات ؛ قال :
Kwa ajili hii amesema sheikh l-islam ibn Taimiyyah katika aqidatul-wasitwiyah maneno katika maneno mazuri mno ,amesema (hivi) :
” من تدبر القرآن طالبا الهدى منه تبين له طريق الحق ” ؛
“mwenye kuizingatia qurani hali ya kutafuta uongofu kutoka humo itambainikia njia ya haki”.
وهذه كلمة مأخوذة من القران منطوقا ؛ ومفهوما.
Maneno haya yamechukuliwa kutoka katika quran kimatamko na kiufahamu.
📚تفسير القران الكريم (٢٨٦/٣)
Maelezo ya mwandishi:
Allah hamuongozi mtu dhalimu na hampi taufiki ya kuifahamu haki na kuifanyia kazi, ina maana mtu muadilifu Allah -aliyetukuka-humuongoza na kumuonesha njia ya uongofu, na qurani imeteremshwa ili kuwaongoza watu basi yeyote mwenye kutafuta uongofu kutoka katika quran Allah atamuongoza kinachotakiwa ni mja kumuelekea Allah kwa kweli na kama atakuwa mkweli basi Allah atamuongoza.
Mwandishi : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 10, 1443H ≈ Feb 11, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•