FAIDA KUTOKA KATIKA QURANI

Makala namba (3)

قال الله تعالى :

Amesema Allah aliyetukuka:

﴿إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَيَجْعَلُ لَهُمُ الرَّحْمَٰنُ وُدًّا﴾

Hakika wale walioamini na wakafanya mema (Allah) Mwingi wa rehema atawafanyia mapenzi

“مريم: ٩٦”

قـال العلامــة عــبدالــرحمــٰن الســعدي رحمه الله:-

Amesema mwanachuoni mkubwa Abdul-Rrahman Assa’adiy-Allah amrahamu-:

«هـذا مـن نعمـه عـلى عبـاده، الذيـن جـمعوا بيـن الإيمـان والعـمل الـصالح، أن وعـدهم أنه يجـعل لهـم وداً، أي: مـحبة ووداداً فـي قلـوب أوليــائه،وأهل السماء والأرض

Hii ni katika neema zake juu ya waja wake ambao wamekusanya baina ya imani na matendo mema (Allah) amewaahidi kuwa yeye atawawekea mapenzi kwa maana mahaba makubwa katika nyoyo za mawalii wake wambinguni na waardhini

وإذا كــان لــهم فـي الـقلوب ودٌ تيــسر لهـم كثـيرٌ مــن أمورهــم وحصــل لـهم مـن الخيــرات والدعــوات والإرشــاد والــقبول والإمامــة مــا حــصل»

Na wakiwa wana mapenzi katika nyoyo (za waja wema), huwa mepesi mambo yao mengi na hupatikana kwao heri na dua na miongozo na kukubalika (na watu) na (kupewa) uongozi

“تفسيــر الــسعدي(ص٥٠١)”

Maelezo ya muandishi :

Katika alama zinazoonesha kuwa mja amependwa na Allah ni kupendwa na waumini kama ilivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:

( إِنَّ اللَّهَ -تَبَارَكَ وَتَعَالَى- إِذَا أَحَبَّ عَبْدًا نَادَى جِبْرِيلَ:

Hakika Allah -aliyezidi heri na kutukuka-pindi anapompenda mja humuita Jibril:

إِنَّ اللَّهَ قَدْ أَحَبَّ فُلَانًا فَأَحِبَّهُ، فَيُحِبُّهُ جِبْرِيلُ، ثُمَّ يُنَادِي جِبْرِيلُ فِي السَّماء:

Hakika Allah bila shaka amempenda (mtu) fulani basi (ewe Jibril) mpende (mtu) huyo,basi Jibril humpenda (mtu) huyo kisha Jibril hunadi mbinguni (kwa kusema) :

إِنَّ اللَّهَ قَدْ أَحَب فُلَانًا فَأَحِبُّوهُ، فَيُحِبُّهُ أَهْلُ السَّمَاءِ، وَيُوضَعُ لَهُ الْقَبُولُ فِي أَهْلِ الْأرَْضِ ) ……

Hakika Allah bila shaka amempenda (mtu) fulani basi (na nyinyi) mpendeni basi humpenda (viumbe) wambinguni, na (Allah) humfanya kuwa ni mwenye kukubalika kwa watu duniani…

رواه البخاري.
Ufafanuzi:

Hadithi ipo wazi kabisa katika kubainisha kuwa pindi Allah anapompenda mtu humuita Jibril na kumwambia ampende mtu huyo kisha Jibril huwaambia wakazi wa mbinguni wampende mtu huyo na Allah humfanya mtu huyo kuwa ni mwenye kupendwa na watu wema : waumini na mawalii wake yaani vipenzi vyake, na walii maana yake ni kila muumini mcha Mungu.

Tanbih:

Mtu huyu hupendwa na waumini wacha Mungu ama waovu kama washirikina, makafiri,wazushi hawa hawazingatiwi kwa sababu ni kawaida yao kuwafanyia uadui watu wema.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 10, 1443H ≈ Feb 11, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *