makala namba (11) .
قال الله تعالى :
وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ
Amesema Allah -aliyetukuka -:
{ Na kaa nao kwa wema duniani }
سورة لقمان ١٥
قــال العلامة ابـن عثيمــين رحمه الله:-
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin -Allah amrahamu -:
«… أن فُـسُوقَ الوالـدَيْن وكُفْرَهُـمَا لا يُسْـقِطُ حَقَّهُـمَا مِـنَ البِـرِّ، يُؤْخَـذ ذلـك مِـنْ قَـوْلِه تعالـى:-
Hakika uovu wa wazazi wawili na ukafiri wao havidondoshi haki yao katika wema (na) hilo linachukuliwa katika kauli yake (Allah) aliyetukuka-:
﴿وَصَاحِبْهُـمَا فِـي الـدُّنْيَا مَعْــرُوفًا﴾،
{Kaa nao kwa wema hapa duniani}
فإنَّـه أَمَـر بِمُـصَاحَبَتِهَـما مَعْـرُوفًا مَـع أنَّهُـمَا كَافِرَيْـن ويَأمُـرَان بالكُــفْر».
Basi bila shaka yeye (Allah) ameamrisha kusuhubiana nao kwa wema pamoja kwamba hao (wazazi) wawili ni makafiri na wanaamrisha ukafiri.
“تفسير سـورة لقمــان ( ٩٧)”.
Maelezo ya mfasiri:
Haki ya wazazi wawili ni nzito sana kiasi ambacho hata kama watakuwa ni makafiri na wakamuamrisha mtoto ukafiri mtoto anatakiwa asiwatii katika hiyo amri na mengineyo katika maovu lakini haki yao ya kuishi nao kwa wema inabakia palepale.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shabani 4, 1443H ≈ Mar 7, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•