Makala namba (14)
قال العلامة ابن عثيمين -رحمه الله- :
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimini -Allah amrahamu -:
⚠️ الإنسان إذا لم يحرص على علاج مرض قلبه فإنه يُعاقب بزيادة المرض.
Binadamu kama hakupupia kuyatibu maradhi ya moyo wake basi hakika yeye huadhibiwa kwa kuzidishiwa (hayo) maradhi.
قال الله عز وجل :
Amesema Allah aliyetukuka -:
{ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ ٱللَّهُ مَرَضًا ۖ }
{ Nyoyoni mwao mna maradhi, na Allah akawazidishia maradhi }
البقرة ١٠
لا شك أن هذه العقوبة أعظم من العقوبة بفقد الولد و الأهل و المال .
Bila shaka kuwa hii adhabu ni kubwa zaidi kuliko adhabu ya kumkosa mtoto na mke na mali.
و كثير من الناس يغفل عنها
Na wengi katika watu wanaghafilika na hilo
فكثير من الناس ، يظنون أن العقوبة إنما تكون في الأمور الظاهرة كالأبدان و الأموال و الأولاد .
Basi wengi katika watu wanadhani kuwa adhabu huwa katika mambo ya dhahiri kama (katika) viwiliwili na mali na watoto.
و الحقيقة : أن العقوبة بمرض القلوب و فسادها أشد و أعظم من العقوبة بمثل تلك الأمور ،
Na kwa hakika : Kuwa kuadhibiwa kwa maradhi ya moyo na kuharibika kwake hizo (nyoyo) ni (jambo) zito zaidi na kubwa zaidi kuliko kuadhibiwa kwa mfano wa vitu hivyo (ufakiri, kufiwa n.k)
بل إن كثيراً من الناس يكون قلبه ميتاً يصاب بالمصائب من الخوف و الجوع و غير ذلك من المصائب المادية المحسوسة
Bali hakika wengi katika watu (kuna yule ambaye) moyo wake unakuwa umekufa ,hupatwa na masaibu kama vile hofu,njaa na mengineyo yasiyokuwa hayo katika masaibu ya vitu (mbalimbali) yanayoonekana
و لا يرعوي و لا يرتدع عما هو عليه من الفسوق و العصيان “
Na wala (mtu huyu) hajizuii na kukemeka kwa kuyaacha aliyokuwa nayo katika maovu na maasi.
📚 [أحكام القرآن لابن عثيمين (١/٧٨٨).
Maelezo ya mfasiri :
Maradhi ya moyo ni maradhi ya shubha (utata) ambayo ndani yake hukusanyika maradhi mbalimbali kama unafiki, shaka, n.k na aina ya pili ya maradhi ni maradhi ya shahwa (matamanio mabaya) ambayo ndani yake kuna maradhi mbalimbali kama kama vile uovu wa liwati, uzinifu, ulevi n.k.
Kama alivyosema sheikh -Allah amrahamu -kuwa mtu kupata mitihani mbalimbali ya kiulimwengu hilo ni jambo jepesi kwake kama vile kupatwa na maradhi ya mwili au kufilisika au kufiwa, ama balaa kubwa zaidi ni mtu kupatwa na maradhi ya moyo yaani mtu akawa amezama katika maovu mbalimbali pamoja na mitihani anayopewa ili ajirudi na kutubu kwa Allah kwa sababu ya madhambi yake lakini yeye akawa hahisi chochote kwa sababu ya maradhi ya moyo aliyokuwa nayo!
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 1, 1443H ≈ May 31, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•